Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi leo amefunga
kozi ya waamuzi chipukizi wasiokuwa na beji za FIFA katika hoteli ya
Holiday, ambapo jumla ya waamuzi 30 kutoka nchi 28 barani Afrika
walihudhuria.
Akiongea
wakati wa kufunga kozi hiyo Malinzi alitoa wito kwa wahitimu wajikite
kwenye maadili kwa kuzingatia mafunzo waliyopata ili katika kipindi
kifupi wote wapate beji za FIFA na waonekane kweye mashindano makubwa
kama fainali za AFCON na mashindano ya Kombe la Dunia.
Kabla ya
Hotuba ya Mgeni rasmi mwakilishi wa CAF Eddy aliishukuru TFF kwa
maandalizi mazuri na usimamizi bora kwa kipindi chore cha kozi hii, na
kuahidi kuleta kozi nyingine kubwa hapa nchini.
Naye
mwakilishi wa FIFA Carlos Hendrique alitoa shukurani zake za dhati kwa
TFF kwa kuwa tayari wakati wote kushirikiana na FIFA hali ambayo
imefanyika TFF iaminike na itegemewe na FIFA kweye program mbalimbali
Kozi hiyo ya waamuzi imefanyika kwa mara ya kwanza hapa barani Afrika.
FIFA
iliiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa kozi hii kwa nchi zinazo zungumza
kiingereza. Kwa upande wa nchi zinazo zungumza kifaransa kozi ya aina
hii imefanyika nchini Morocco
Washiriki 30 kutoka nchi 28 barani Afrika wamehudhuria kozi hii ilivyokuwa itafundishwa na Wakufunzi wa Sita kutoka CAF na FIFA.
0 comments:
Post a Comment