Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amemshukuru Rais wa CECAFA, Leodgar Tenga kwa
kuipa Tanzania uenyeji wa mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) iliyomalizika jana kwa klabu ya Azam FC kutawazwa Mabingwa wapya wa michuano hiyo.
kuipa Tanzania uenyeji wa mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) iliyomalizika jana kwa klabu ya Azam FC kutawazwa Mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Aidha
Malinzi ameishukuru Kamati ya Ndani ya Uendeshaji ya Michuano hiyo
(LOC) kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuandaa na kuhakikisha michuano
hiyo inafanyika na kumalizika katika hali ya usalama na amani.
Malinzi
pia amewapongeza wapenzi, washabiki na wadau wa soka nchini
waliojitokeza kushuhudia michezo ya michuano hiyo na kuonyesha nidhamu
ya hali ya juu ndani nan je ya uwanja kipindi chote cha michuano.
Rais
Malinzi ameipongeza klabu ya Azam FC kwa kutwaa Ubingwa Kagame, kwa
kutwaa ubingwa huo imeweza kuweka historia ya kutwaa Ubingwa huo kwa
mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake na pia kuwa klabu iliyocheza
michuano hiyo na kuwa Bingwa bila kuruhusu nyavu zake kutikisika.
Pia
Malinzi amewashukuru waandishi wa habari/vyombo vya habari kwa sapoti
yao wakati wa michuano hiyo. Shukrani hizo pia zimepelekwa kwa klabu za
Yanga SC, KMKM kwa kushiriki mashindano hayo.
U-15 YAREJEA KUTOKA ZANZIBAR
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15),
kimerejea leo asubuhi kutokea kisiwani Zanzibar kilipokwenda kucheza
michezo ya kujipima nguvu na kombani ya U-15 ya kisiwani humo.
Katika
michezo miwili iliyocheza kisiwani humo, iliweza kushinda michezo yote
miwili, (4-0 ), (1-0), huku kocha Bakari Shime akiwapongeza vijana wake
na kusema wanaendelea kuimarika kuelekea kujiandaa na kuwania kufuzu
kwa fianali za Mataifa Afrika chini ya miaka 17 mwakani.
Baada
ya kurejea jijini Dar es salaam leo, kambi ya timu hiyo imevunjwa na
vijana hao watakutana tena mwisho wa mwezi wa Agosti kama ilivyo katika
program yao ya kukutana kila mwisho wa mwezi na kucheza michezo ya
kirafiki.
Mwishoni
mwa mwezi Agosti timu hiyo ya vijana inatarajiwa kuelekea mkoani Tanga
kucheza michezo ya kirafiki na kombani ya mkoani humo, ambapo kocha wake
Shime pia anatumia nafasi hiyo kutazama wachezaji wengine wenye uwezo
mzuri katika timu za kombaini za mikoa kwa ajli ya kuwaongeza katika
kikosi chake.
Mpaka
sasa timu hiyo ya vijana chini ya miaka 15 (U15) imeshafanya ziara na
kucheza michezo katika miji ya Mbeya na kisiwani Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment