Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha kupitia chama cha CUF Salussingo Omari akizungumza na vyombo vya habari.
|
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ni mgombea
Urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)anatarajiwa
kupokelewa kwa mapokezi makubwa ikiwemo magari,pikipiki,katika uwanja
wa ndege wa kia hadi viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini
Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15) ambapo atahutubia wananchi
katika mkutano ulioandaliwa na chama hicho.
Akizungumza mapema jana
na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho juu ya maandalizi
hayo Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alisema kuwa
mapokezi hayo yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukiohilo ni la
kihistoria Alisema kuwa lengo la ujio huo ni kumtambulisha mgombea
urais ambaye ataambatana na mgombea mwenza Juma Duni Hajji ,kwa
kuwatambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha sambamba na kupata
udhamini wa wananchama waliojiandikisha kupiga kuraPia alisema kuwa
zoezi la udhamini umeshaanza Arusha na uongozi wa Tume umaelekeza
mgombea kupata wadhamini 300 na jimbo la Moshi mjini wataoa wadhamini
300.
Aidha aliwataka ,wakazi wa jijili la Arusha na waliopo jirani kujitokeza kwa wingi katika tukiohilo la kihistoria ambapo pia viongozi wakuu wa chama hicho watahudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,wenyeviti wenza wa ukawa kutoka NLD,NCCR pamoja na chama cha CUF,John Mnyika ,Nibu katibu mkuuZanzibar Salum Mwalimu na viongozi wengine wengi“Kwakushirikiana na jeshi la polisi pamoja na vikosi vyetu suala la Amani,Utulivu,Ulinzi na Usalama vitadumishwa katika msafara huo pamoja na mkutano huo”Alisema GolugwaHata hivyo baada ya mkutano huo kuisha msafara huo utaelekea katika jimbo la Monduli ambapo pia Mh.Lowassa atapata wasaa wa kuhutubia wananchi katika jimbo hiloKwa upande wake Naibu katibu mkuu waTimu Lowassa for president Ndama Jeuri alisema wamejiandaa vizuri kumpokea na wataendelea kuhamasisha watu kumuunga mkono Lowassa katika harakati zake za Urais.
Katika msafara huo zaidi ya magari 75 yataanzia katika ofisi za chadema hadi katika uwanja wa ndege wa kia huku vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Lowassa.
Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mapokezi ya mgombea Urais Edward Lowassa kupitia CHADEMA yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukio hilo kuliita la kiistoria ambalo litafanyika katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15)
0 comments:
Post a Comment