Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu ya mpira ya wilaya ya Ilemela inayotaraji kushiriki mashindano ya UMISETA mkoa wa Mwanza hivi karibuni
Akizungumza kwa niaba ya Mhe mbunge katibu wa ofisi ya mbunge Komredi Kheri James amesema
‘… Mbunge wetu ni mwana michezo hivyo ameona ni vyema ashiriki nanyi kwa kuunga mkono mashindano ya UMISETA hapa wilayani kwetu na kuamini kuwa michezo ni afya na michezo ni ajira hivyo niwasihi walimu na wadau wa michezo kuwatengenezea kesho yao yenye kipato na afya…’ Alisema
Aidha Mhe Mbunge ameendelea kuwa balozi bora wa michezo jimboni kwa yeye mwenyewe kucheza lakini pia kwa kugawa vifaa vya michezo katika Klabu na mashule mbalimbali, kuanzisha ligi ya jimbo na kufungua fursa za uwekezaji mkubwa wa michezo kupitia taasisi na asasi za nje ya nchi
Nae afisa Michezo wa manispaa ya Ilemela Kizito Sosho Bahati amesema kuwa manispaa ya Ilemela itaendelea kushirikiana na mbunge huyo kuhakikisha wanaboresha michezo na kuiletea sifa Ilemela ikiwa ni sambamba na kuboresha maisha yao kwa kujipatia ajira
Kwa upande wao wanafunzi walioshiriki makabidhiano hayo wamemshukuru Mbunge huyo kwa jitihada zake anazozifanya ikiwemo ya ukuzaji wa michezo ndani ya jimbo lake huku wakimuhakikishia kufanya vizuri katika mashindano hayo na kumuunga mkono katika shughuli zote za maendeleo
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
25.05.2017
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
25.05.2017
0 comments:
Post a Comment