METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 14, 2015

BVR MARUDIO MWISHO LINI?




Tokakutangazwa na tume ya uchaguzi kuwa ukaguzi wa majina kwenye daftari la kudumu la mpiga kura lifanyike kwenye ofisi za kata zote za nchi nzima zoezi hilo lililopangwa pia kufanywa siku 5 kwa kila halmashauri baadhi ya halmashauri zimehitimisha zoezi hilo kwa uhakiki na kubadili vitambulisho kwa watu waliohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wale waliopoteza vitambulisho hivyo au kuvivunja.
Manispaa ya Iringa imemaliza zoezi hilo ingawa wananchi wengi wao wakiwahawatambui uwepo wa zoezi hili katika manispaa hiyo akiwepo Katibu wa ccm halmashauri ya iringa na baadhi ya wafanyakazi wakiwapo wafanyakazi wa maofisini kutokana na zoezi hilo kufanywa siku za kazi.
Wakizungumza na wazohuru baadhi ya wananchi akiwapo Katibu Muhtasi wa chuo kikuu iringa amesema haelewi kama kunazoezi hilo pia hao maana ya kufika katika kuthibitisha jina ikiwa kitambulisho anacho hivyo anaisubiri siku hiyo ya kupiga kura.
Kwaupande wa halmashauri ya Iringa zoezi hilo siku tano za awali zilitosha kuthibisha majina kutokana na umbali wa kijiji na kijiji hadi kufikia ofisi ya kata wananchi hao waliwasilisha matatizo ya na zoezi la kubadili vitambulisho linaendelea katika halmashauri hiyo wakati mpaka kufikia hii leo wameweza kuandikisha katika kata 15 kati ya kata 28 ambapo siku ya jana ambayo zoezi hilo lilianzia katika kata za malenga makali na Ifunda katika kata ya Ifunda wanafunzi kutoka katika shule ya Tosamaganga na Ifunda Teck wanaotegema mpaka siku ya uchaguzi watakuwapo shuleni hapo walibadili vitambulisho zaidi ya 150 ikiwa halmashauri inamashine 6 tuu.
“Zoezi hilo mpaka sasa halijatambulika litakamilika lini kutokana na kusubiri tamko kutoka tume” Hayo yalisemwa na Afisa uchaguzi wa halmashauri ya Iringa hii leo huku akisema linataraji kuendelea kutoka na muundo wa halmashauri ulivyo kesho wanataraji kufika katika kata za Magulilwa,kissing’aIgingilanyi na zilizopo jilani.
Kutokana na zoezi hilo linaloendelea wananchi wa manispaa ya iringa wametoa ushauri kwa tume kushirikisha jamii kila hatua inayofuata ili kuepusha usumbufu kwa wasimamimizi siku ya uchaguzi na kuondokana na vurugu ambazo huenda zikatokea kwenye vituo pindi  ambapo baadhi ya majina yatakapokosekana, Hii inatokana na siasa za uchaguzi huu zilivyo na hamasa kubwa dhidi ya vyama vinavyohitaji kupata madalaka ya kuongoza jamii husika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com