Tokakutangazwa na tume ya uchaguzi kuwa ukaguzi wa majina kwenye daftari la kudumu la mpiga kura lifanyike kwenye ofisi za kata zote za nchi nzima zoezi hilo lililopangwa pia kufanywa siku 5 kwa kila halmashauri baadhi ya halmashauri zimehitimisha zoezi hilo kwa uhakiki na kubadili vitambulisho kwa watu waliohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wale waliopoteza vitambulisho hivyo au kuvivunja.
Manispaa ya Iringa imemaliza zoezi hilo ingawa wananchi
wengi wao wakiwahawatambui uwepo wa zoezi hili katika manispaa hiyo akiwepo
Katibu wa ccm halmashauri ya iringa na baadhi ya wafanyakazi wakiwapo
wafanyakazi wa maofisini kutokana na zoezi hilo kufanywa siku za kazi.
Wakizungumza na wazohuru baadhi ya wananchi akiwapo Katibu Muhtasi wa
chuo kikuu iringa amesema haelewi kama kunazoezi hilo pia hao maana ya kufika
katika kuthibitisha jina ikiwa kitambulisho anacho hivyo anaisubiri siku hiyo
ya kupiga kura.
Kwaupande wa halmashauri ya Iringa zoezi hilo siku tano za
awali zilitosha kuthibisha majina kutokana na umbali wa kijiji na kijiji hadi
kufikia ofisi ya kata wananchi hao waliwasilisha matatizo ya na zoezi la
kubadili vitambulisho linaendelea katika halmashauri hiyo wakati mpaka kufikia
hii leo wameweza kuandikisha katika kata 15 kati ya kata 28 ambapo siku ya jana
ambayo zoezi hilo lilianzia katika kata za malenga makali na Ifunda katika kata
ya Ifunda wanafunzi kutoka katika shule ya Tosamaganga na Ifunda Teck
wanaotegema mpaka siku ya uchaguzi watakuwapo shuleni hapo walibadili vitambulisho
zaidi ya 150 ikiwa halmashauri inamashine 6 tuu.
“Zoezi hilo mpaka sasa halijatambulika litakamilika lini
kutokana na kusubiri tamko kutoka tume” Hayo yalisemwa na Afisa uchaguzi wa
halmashauri ya Iringa hii leo huku akisema linataraji kuendelea kutoka na
muundo wa halmashauri ulivyo kesho wanataraji kufika katika kata za Magulilwa,kissing’aIgingilanyi
na zilizopo jilani.
Kutokana na zoezi hilo linaloendelea wananchi wa manispaa ya
iringa wametoa ushauri kwa tume kushirikisha jamii kila hatua inayofuata ili
kuepusha usumbufu kwa wasimamimizi siku ya uchaguzi na kuondokana na vurugu
ambazo huenda zikatokea kwenye vituo pindi
ambapo baadhi ya majina yatakapokosekana, Hii inatokana na siasa za
uchaguzi huu zilivyo na hamasa kubwa dhidi ya vyama vinavyohitaji kupata
madalaka ya kuongoza jamii husika.
No comments:
Post a Comment