
Wachezaji
wa timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam wakisherehekea ubingwa wao
wa Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, mara baada ya kuitungua timu ya Gor
Mahia ya nchini Kenya Bao 2-0, katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja
wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo.

Balozi
wa Rwanda nchini Tanzania,Mhe. Eugene Segore Kayihura (wa pili kulia)
akikabidhi kitita cha Dola za Kimarekani eflu 30 kwa Nahodha wa Timu ya
Azam FC, John Bocco "Adebayor" ikiwa ni zawadi ya ushindi wa kwanza
iliyotolewa na Mdhamini Mkuu wa Mashindao hayo ambaye ni Rais wa Rwanda,
Mh. Paul Kagame. Wengine pichani toka kushoto ni Rais wa Cecafa,
Leodger Tenga, Mgeni Rasmi kwenye Mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mh. Said Meck Sadick, Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh.
Raila Odinga pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Mgeni
Rasmi kwenye Mchezo fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame Cup 2015,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia)
akishirikiana na Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh. Raila Odinga
wakimkabidhi Kombe la Ubingwa huo, Nahodha wa Timu ya Azam FC, John
Bocco "Adebayor" baada ya kuichapa bao 2-0 timu ya Gor Mahia ya nchini
Kenya katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es
salaam leo.

Kiungo
hodari wa Timu ya Azam FC, Ammy Ali akiondika na mpira huku Mabeki wa
Timu ya Gor Mahia wakiangalia namna ya kumdhibiti, katika mtanange wa
fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao
2-0 na kutwaa ubingwa huo.

kiungo wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Karim Nizigiyimana akiachua shuti kuelekea lakongoni mwa timu ya Azam FC.
0 comments:
Post a Comment