Waziri wa fedha nchini Ugiriki
ametoa taarifa siku moja kabla ya kuandaliwa kwa kura ya maoni juu ya
mpango wa kulipa deni lake.
Kwenye mahojiano na gazeti la El Mundo
nchini Uhispania Yanis Varoufakis aliwalaumu wakopeshaji wa nchi kwa
kile alichokitaja kuwa ugaidi akisema kuwa wanataka kura ya ndio ili
waweze kuidhulumua Ugiriki.Aliongeza kuwa mabenki nchini Ugiriki yatafunguliwa siku ya Jumanne bila kujali matokeo ya kura hiyo.
Mapema pande mbili kwenye kura hiyo ya maoni zilimaliza kampeni zao kwa mikutano mikubwa.
Waziri mkuu Alexis Tsipras amesema kuwa kukataa kura hiyo kutamwezesha kupata makubaliano mazuri na wakopeshaji wa nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment