RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuongoza mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu katika sala ya Idd el Fitr itakayofanyika kimkoa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Sala ya Idd inatarajiwa kuswaliwa kati ya siku ya Ijumaa au Jumamosi, kwa kutegemea mwandamo wa mwezi ambapo sala hiyo kitaifa itafanyika katika mkoa wa Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sikukuu hiyo, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema, kimkoa sala hiyo itafanyika katika viwanja hivyo saa 1:30 asubuhi ambapo pia itahudhuriwa na viongozi wengine akiwemo Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal.
“Sikukuu ya Idd ni siku ya furaha kwa wote, Zakatul Fitr itolewe kabla ya swala ya Idd kuswaliwa, yatima, wajane, mafakiri na masikini wakumbukwe kwa misaada mbalimbali, wagonjwa watembelewe na kufarijiwa na waliogombana wapatane,” alisema Shehe Salum.
0 comments:
Post a Comment