Mgombea ubunge jimbo
la Ismani Mh. Festo Kiswaga
Baada ya zoezi la uchaguzi
wa wagombea urais kukamilika katika vyama sasa zoezi limeanza kwa wabunge na
madiwani ambapo hii leo Festo Kiswaga ambaye ameweka nia ya kugombea katika
jimbo la isiman.
Katika mkutano huo na
waandishi wa habari KIswaga amekanusha uvumi uliokuwa umezagaa juu ya kuhongwa
pesa mwaka 2010 ili kutogombea huku akidai kuwa alishindwa kwa haiki na si
hongo ya mbunge aliyepo madalakani kwasasa huku akimzawadia ukuu wa wilaya.
Ambapo pia ametumia mkutano
huo ili kuujulisha uma juu ya maelengo yake ya kuchukua form katika wasifu wake
amesema anadigree ya sayansi ya wanyama poli na kutumikia katika shirika la
mbomipa na kuwatumikia wananchi wa misenyi mkoa wa kagera akiwa ni mkuu wa
wilaya na sasa ni mkuu wa wilaya ya Nanyumbu huku akitumikia mashirika kama
tanapa na chuo kikuu cha dar es-laam na kuteuliwa kuwa rais wa wa shirikisho vyuo
vikuu vya umoja wa Afrika mashariki uliojumuisha vyou vikuu zaidi ya 400 katika nchi za Tanzania,Uganda,Kenya na
Burundi.
Akizungumzia kuhusu janga la
njaa lililopo katika jimbo hilo amekiri kuwa anauzoefu juu ya utatuzi wa
matatizo kama hayo kutokana na nyanja mbalimbali ambazo amepitia na pia
amewataka wananchi wa ismani kumpa lidhaa yya kuwaongoza kutokana tatizo kama
hilo amelikuta katika wilaya ya Namnyumbu na akafanikiwa kulitatua kwa asilimia
100%.
Aidha amesema kutokana na
jimbo hilo kukosa kiongozi mwenye uchungu kama yeye imepelekea kukosekana kwa
huduma kama maji katika vijiji mbalimbali ikiwa jimbo hilo limefikisha miaka 20
ikiwa mashirika mbalimbali na serikali licha ya kuchangia lakini ukosefu wa
maji umekuwa tatizo si kwa binadamu tuu bali hata kwa mifugo ambapo hupelekea
wananchi kununua maji hadi kwa shiringi mia 500.
Kwaupande wa wananchi
waliohudhulia mkutano huo wamekiri kuwapo kwa tatizo hilo ambalo imekuwapo kwa
miaka mingi sasa hali inyopelekea wananchi upeleka mifugo yao kunywesha usiku
wa manane hali ambayo ineza kuhatarisha usalama wa mifugo hiyo.
Nao kinamama wamekiri kuwa
tatizo hilo limekuwa likiwaathiri kiuchumi kwakuwa hutumia muda mwingi katika
kutafuta maji bila kufanya shughuli nyingine kwaajiri ya kujenga uchumi wao na
wanchi.
0 comments:
Post a Comment