METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 16, 2015

JK aongoza vikao jopo la magonjwa ya milipuko

Rais Jakaya Kikwete.Rais Jakaya Kikwete.

RAIS Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa linalochunguza jinsi dunia inavyoweza kujikinga na majanga ya magonjwa ya milipuko katika miaka ijayo, yuko jijini hapa kuanzia juzi usiku kwa ajili ya kuendesha vikao vya jopo hilo.

Vikao hivyo vitakuwa ni awamu ya pili kwa jopo hilo ambalo liliteuliwa Aprili mwaka huu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki moon.

Wajibu mkuu wa jopo hilo ni kutoa mapendekezo ya kuimarisha mifumo ya kitaifa na kimataifa, ili kuweza kuzuia ama kudhibiti kwa uhakika zaidi majanga ya magonjwa ya milipuko kufuatia balaa la ebola katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea ambalo limeua maelfu kwa maelfu ya watu.

Jopo hilo lilifanya vikao vyake kwa mara ya kwanza Mei, mwaka huu, katika makao makuu ya UN mjini New York, Marekani. Vikao vya sasa vilivyoanza juzi, vitachukua siku tano na vitafanyika kwenye Ofisi za UN na zile za Shirika la Umoja wa Mataifa ya Afya (WHO) mjini Geneva.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com