Dodoma. Zikiwa zimesalia siku nne, kabla ya kumalizika kwa uchukuaji na urudishaji fomu za kuwania urais CCM, kada wa chama hicho Banda Sonoko (46) amechukua fomu akijigamba kwamba yeye ni greda linalokuja kusawazisha nchi.
Wagombea wote wanatakiwa kumaliza michakato yao
ndani ya wiki hii na hadi kufikia Ijumaa, kila mmoja awe amewasilisha
vielelezo vyake ikiwamo majina ya wadhamini 450 kutoka mikoa 15, kati ya
hiyo mitatu ya Zanzibar kupisha vikao vya kujadili na kuchuja wagombea
vitakavyofanyika kuanzia mwishoni mwa wiki ijayo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu, Sonoko
ambaye anakuwa kada wa 42 wa CCM kuchukua fomu alisema ameamua kufanya
hivyo kwa sababu anazo sifa, vigezo na uwezo kwamba ndiye anayeweza
kuvaa viatu vya Mwalimu Julius Nyerere... “na hivi viatu sina haja ya
kuvifuata Mwitongo (Kijiji alichozaliwa Mwalimu), hivi viatu anavyo
mchezaji mmoja, aliwahi kucheza aliwahi kucheza nchini hapa. Huyo
mchezaji alipocheza alifunga magoli mengi sana na kama Taifa,
tukafaidika. Hivi viatu havijakwenda Mwitongo, sihitaji kwenda Butiama,
anavyo mtu fulani ni kiasi tu cha kwenda na kumwambia naomba viatu hivi
nivivae. Kilicho kizuri ni kwamba navifahamu mpaka na namba na alama
zake. Kiatu cha kulia cha Mwalimu Nyerere kina alama mbili ya kwanza ni
nchi kujiendesha kwa kodi zetu. Kodi hizi zitathiminiwe, zidaiwe kwa
muda na hilo liwe jambo la msingi, misaada iwe suala la mjadala,”
alisema.
Alisema nchi ina raslimali nyingi za kutosha na kinachotakiwa ni usimamizi katika eneo hilo.
Alisema CCM imefanya mambo makubwa katika uongozi
wake ikiwamo kutengeneza miundombinu ya kutosha na sasa kinachotakiwa
kuisawazisha... “Miji yetu imeshakaa vizuri sasa nchi yetu inahitaji
greda liweze kusawazisha… na greda ni mimi, nitaweza kusawazisha
matatizo yaliyobaki na kuweza kuhakikisha lindi la umaskini
linaondolewa.”
Sonoko alisema rais anayehitajika kwa wakati huu ni yule anayejali muda na kuwa na uamuzi, mambo ambayo yote anayo.
Alisema kaulimbiu yake ni kutokomeza umaskini na kwamba anaamini katika usimamizi jambo hilo mkazo endapo atafanikiwa kuwa rais.
Vipaumbele vingine ni kufufua uchumi wa viwanda,
kuwekeza katika uchumi wa kilimo na kwamba tangu alipoondoka, Mwalimu
Nyerere hakuna kiongozi ambaye amekuwa tayari kuimba wimbo wa kuboresha
kilimo.
Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, amesema CCM na Serikali yake, haviwezi
kutishwa na mtu yeyote katika kutekeleza uamuzi wowote kutokana na kuwa
na historia, msimamo usioyumba na uongozi thabiti.
Akizungumza na wanachama wa CCM wa mkoani Kigoma
waliofika kumdhamini juzi, Membe aliwataka Watanzania wakatae vitisho na
ulaghai kutoka kwa mtu yeyote katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa
mwaka huu.
“Ole wao ama ole wake mtu yeyote atakayejitia
kuleta bughudha pale eti kwa kisingizio kwamba eti chama hakikuchukua
hatua sahihi. Nataka kuwaambia, wajumbe wa Mkutano Mkuu ni watu makini
sana.
0 comments:
Post a Comment