Baadhi ya wananchi wakiwa katika chumba cha usajili tayari kusajiliwa.
Hawa ni baadhi tu ya wananchi
waliojitokeza katika zoezi la Usajil Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya
Kilolo mkoa wa Iringa. Kwa sasa zoezi hili linafanyika kwa awamu ngazi
ya Kata ili kutoa fursa kwa wananchi wote wenye sifa kusajiliwa.
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa akiingiza taarifa za wananchi kwenye mfumo kabla ya kuchukua
taarifa za kibaiolojia za wananchi wa Kilolo ambako zoezi kwa sasa
linaendelea.
Mmoja wa wananchi akichukuliwa alama za
vidole na saini ya kielektroniki ikiwa ni hatua muhimu kabla ya
kukamilisha hatua za Usajili Vitambumnbulisho vya Taifa. Mkoa wa Iringa
ni moja ya Wilaya zinazo endelea na Usajili kwa sasa kati ya mikoa 11 ya
Tanzania.
Wananchi wa Wilaya ya Kilolo wameendelea
kujitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa baada ya
kukamilisha awamu ya kwanza ya usajili ambayo ni kujaza fomu za maombi
ya Usajili na fomu zao kupitishwa na Serikali za Vijiji wanakoishi.
Zoezi linaenda sambamba na uhakiki wa
taarifa za wananchi wanaoomba kupewa vitambulisho vya Taifa chini ya
Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya Mitaa na Vijiji kabla ya kutoa
nafasi kwa wananchi kuweka Mapingamizi ya wazi kwa wale waombaji
wanaotiliwa shaka uraia wao kabla ya kuendelea na mchakato wa
Uzalishaji.
Wilaya ya Kilolo ni Wilaya ya mwisho
kukamilisha zoezi hili kwa mkoa wa Iringa na hivyo kutoa fursa ya kuanza
kwa matumizi ya Vitambulisho vya Taifa kielektroniki.
Mbali na Iringa mikoa mingine
inayoendelea na zoezi hilo ni ya Kanda ya Ziwa ikiwemo; Geita,
Shinyanga, Mwanza, Manyara na Singida.
0 comments:
Post a Comment