METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 22, 2015

KATIBU MKUU KIONGOZI ATEMBELEA BANDA LA MAMBO YA NJE KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Habu Mkwizu. 
Balozi Sefue akisaini Kitabu cha Wageni katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Balozi Sefue akisoma Kitabu cha Sera ya Mambo ya Nje huku akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya. 
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue (katikati), Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba Yahya (kushoto) wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Habu Mkwizu alipokuwa akiwaelezea jambo. 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake wakifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu mara baada ya Katibu Mkuu Kiongozi kutembelea Banda la Mambo ya Nje. 

Picha na Reginald Philip
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com