MSHAMBULIAJI
wa Yanga SC, Simon Msuva ameng’ara katika usiku wa tuzo za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, baada ya kutwaa kiatu na mpira wa dhahabu.
Katika
hafla ya utoaji tuzo za washindi wa Ligi Kuu msimu uliomalizika Mei
mwaka huu, iliyofanyika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo
katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio, Dar es
Salaam, Msuva amebeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu akiwashinda beki
Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba SC na Mrisho Ngassa waliyekuwa
naye Yanga SC kabla ya kutimkia Afrika Kusini.
Kwa
kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, amepata jumla ya Sh. Milioni 11.4,
yaani Sh. Milioni 5.7 kwa kila tuzo aliyotwaa usiku wa leo. Msuva
ambaye yupo na timu ya taifa, Taifa Stars nchini Ethiopia, aliwakilishwa
na baba yake Happygod Msuva na mama yake Suzan Msuva.
Baba
wa Mzee Happygod Msuva, baba wa mshambuliaji wa Yanga SC, Simon Msuva
(katikati) akiinua tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu kwa niaba
ya mwanawe. Kulia ni Mama Msuva, Susan na kushoto mgeni Rasmi, Waziri
Nkamia.
Kipa
Shaaban Kado wa Coastal Union ameshinda kipa bora wa msimu na kuwabwaga
wenzake Mohamed Yusuph wa Tanzania Prisons na Said Mohamed wa Mtibwa
Sugar kutwaa tuzo hiyo ya kipa bora na kujinyakulia Sh. Milioni 5.7.
Kipa
wa zamani wa Yanga SC, Mbwana Makatta amewashinda Mserbia Goran
Kopunovic aliyekuwa Simba SC na Mholanzi Hans Van Der Pluijm wa Yanga SC
katika tuzo ya kocha bora, baada ya kuinusuru Prisons kushuka daraja na
kuzawadiwa Sh. Milioni 8.6.
Simon Msuva Mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2015-2016
Amewashinda
Jonesia Rukyaa na Samuel Mpenzu katika tuzo ya Mwamuzi Bora na kupata
Sh. Milioni 8.6, wakati Mtibwa Sugar imezipiga kumbo Mgambo JKT na
Simba SC katika tuzo ya timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni
17.2.
Katika
hafla hiyo, mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia alikabidhi hundi ya Sh. Milioni 80.4 kwa kuwa
mabingwa, Azam FC Sh. Milioni 40.2 kwa kuwa wa pili, Simba SC Milioni
28.7 kwa kuwa wa tatu na Mbeya City Milioni 22.9 kwa kuwa nne.
Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kevin Twisa aliwapongeza washindi
wote na akasema wataendelea kudhamini ligi hiyo waliyoanza kuidhamini
mwaka 2002.
Thursday, June 11, 2015
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Timu ya Sevilla FC leo wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya...
-
Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungan...
-
Edson Kamukara enzi za uhai wake Anaandika Mathias Canal, Iringa "Mwandishi wa habari, Edson Kamukara amefariki dunia jana j...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment