Askofu
Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja
amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari
la kudumu la wapiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba na kuchagua
viongozi bora watakaoleta maendeleo ya taifa.
Isanja aliwaasa Watanzania kutozembea nafasi hiyo muhimu na badala yake waitumie fursa hiyo itakayoleta mabadiliko yanayotarajiwa na wengi.
Akizungumza
katika mahafali ya Wahitimu wa Diploma ya masomo ya Biblia amesema kuwa
Tanzania inahitaji Viongozi waadilifu na wenye bidii.
“Watu
wasipige tu kelele barabarani bali wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na
kupiga kura ili kupata viongozi bora watakaoliongoza taifa hili”
Alisema Isanja
Kwa
upande wake Askofu Mwangalizi wa Kanisa hilo Israel Maasa ambaye
alikua mgeni wa heshima katika mahafali hayo amewataka watanzania kuwa
makini na wagombea wanaowagawa Watu kwa misingi ya ukabila na udini na
kutowachagua kwani wataathiri umoja na mshikamano wa kitaifa.
Wilfred
Pallangyo ameeleza kuwa ni wakati wa Watanzania kuwatambua viongozi
watakaofaa kuliongoza taifa na kuwapa nafasi hiyo pasipokufanya makosa
pia kuepuka vitendo vya rushwa hasa tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.
Alisema
kuwa Tayari zoezi la uandikishaji limeanza katika baadhi ya mikoa na
linategemewa kukamilika nchini kote ili kukamilisha uchaguzi utakaoanza
Octoba mwaka huu,vuguvugu la uchaguzi tayari limeanza tumeshuhudia
hekaheka za wagombea wa Urais.(P.T)
0 comments:
Post a Comment