Mashindano hayo yaliyoanzishwa na
Diwani wa kata hiyo Denis Pius Lupala amesema zawadi ambazo zinatolewa
zimelenga kila timu shiriki kupata zawadi ya mpira mmoja mmoja na kwa timu mshindi
wa kwanza atapata Ng’ombe,jenzi na mpira
kwa mshindi wa pili akipata mbuzi, jenzi na mpia pamoja na mshindi wa tatu
akipata jenzi na mpira.
Mashindano hayo yameanza hapo jana
kwa ufunguzi wa mchezo wa timu ya kijiji cha Mgama na Ibumila ambapo timu ya
Mgama imeibugiza Ibumila mabao 2 kwa 1
huku mchezo huo ukitawaliwa na ubabe wa msosi na ufundi mwingi kutoka katika
timu zote mbili.
Na hii leo kutakuwa na mechi mbili
katika vijiji tofauti Ihemi Itakuwa na Ilandutwa Mechi ya pili Itwaga na Lwato.
Muuandaaji wa mashindano hayo Denis
Lupala amewaasa wachezaji kutumia fulsa hiyo ambayo itapelekea kupata timu ya
kata na kuimalisha miili ya kwa kuondokana na magonjwa nyemelezi huku akiahidi
kuongeza mashindano mengine ambayo yatawajenga kiushindani zaidi ilikuongeza
radha ya mashindano hayo, ametoa siku ya 24 ambapo mwenge utalala katika kijiji
hicho kutakuwa na mechi katika timu 6 na kumpata mshindi ambaye yeye atanyakua
Mbuzi,jenzi,na mipia 2 huku mshindi wa pili akipata jenzi na mpia na mshindi wa
Tatu mpia tuu.
Atiba ya mashindano hayo mpaka
mzunguko wa kwanza kuisha ni hii hapa.
0 comments:
Post a Comment