Na Denis Mkakala.
Wananchi wa kijiji cha Ibumila kata ya Mgama Halmashauri ya
Iringa wameilalamikia seikali kwakutomaliza ujeenzi wa Zahanati ya kijiji hicho
ikiwa wao wametimiza ufyatuaji tofali,kukusanya mchanga na kusogeza maji katika
eneo lililoanza kujengwa zahanati hiyo tangu mwaka 2012.
zahanati inayojengwa toka mwaka 2012.
Wakitoamalalamiko yao mbele ya Abraham Kimuli Afisa
Uchechemuzi wa TACOSODE wamesema
kinamama wamekuwa wakizalia njiani wakati wakielekea kupata matibabu katika
kituo cha afya cha ifunda ,hospitali ya Ipamba na hata katika hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Iringa ikiwa nipamoja na baadhi ya akinamama ambao hupata
madhara ya kubakiwa na baadhi ya vitu ndani ya miiliyao baada ya kujifungua.
mwenyekiti wa kijiji cha Ibumila RICHARD MHEMA Akiwa na wananchi katika zahanati inayoendelea kujengwa kijijini hapo.
Akitoaelimu baada ya malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho Afisa Uchehchezi Bw. Kimuli amesema jamii
inapaswakutambua kuwa swala la ujenzi wa majengo ya umma wananchi wao
wanatakiwa kusimamisha jingo mpaka kufikia eneo la bimu ambapo serikali
itachukua jukumu la kuimalizia na kukamilisha ikiwapo na kuweka wauguzi na sio
kuanzaujenzi wa jengo,hivyo ujenzi wa jengo la zahanati hiyo nijukumu lao
wananchi hao na siswala la serikali.
TACOSODE ni mwamvuli wa mashirika yasiyo ya kiserikali wenye
hadhi ya baaza hili pia lina hadhi ya kitaifa,Dira ya Tacosode kuwa asasi zenye
uwezo wa kutetea haki za jamii na Dhamira kuwa na maendeleo endelevu kwa
kujenga uwezo wa rasilimali watu,taasisis na wananchi kwa njia ya mafunzo,uwezeshaji
wa rasilimali na mashiikiano kati ya wadau mbalimbali.
Nae diwani wa kata hiyo ya mgama Denis Lupala amesema ujenzi
huo wa zahanati utakamilika mwezi wa 8 na kuiachia jukumu halmashauri katika
kumaliazia jengo hilo ikiwa nipamoja na ujenzi wa barabara ambayo itatumiwa na
wananchi wakijiji hicho katika kusafiisha mazao yao kupeleka sokoni.
0 comments:
Post a Comment