METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, September 7, 2024

GST NA KIGAM YAANZA MAJADILINO YA AWALI KUHUSU TAFITI ZA MADINI MUHIMU (CRITICAL MINERALS)









Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeanza majadiliano ya awali kuhusu mashirikiano na Serikali ya Korea Kusini kupitia Taasisi ya Jiosayansi na Rasilimali Madini (KIGAM) kwenye tafiti za Madini Muhimu (critical minerals) nchini Tanzania.

Majadiliano hayo, yamefanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia Septemba 5 hadi Septemba 6, 2024 jijini Dodoma. Mazungumzo hayo ni matunda ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Korea Mwezi Juni mwaka huu ambapo Tanzania na Korea zilitia Saini Hati ya Makubaliano ya Mashirikiano katika nyanja za Utafiti na Uongezaji thamani madini nchini.

Aidha, Majadiliano hayo yamehusisha Wataalamu wa Jiolojia kutoka Taasisi ya KIGAM ya nchini Korea na Waatalamu wa Taasisi ya GST ya nchini Tanzania yakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia Dkt. Ronald Massawe.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com