METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 15, 2024

CHIKULUPI NJELU KASAKA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE WA (EALA)

Na Saida Issa, Dodoma  

KUFUTIA Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi kwamba uchaguzi wa mjumbe mmoja atakaye jaza nafasi wazi ya kundi la wanawake kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) ya kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika bunge la Afrika mashariki wanawake wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.  

Akizungumza baada ya kuchukua fomuMgombea wa ubunge Wabunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Chikulupi Kasaka aliishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kukuza umoja na uchumi katika jumuia ya Afrika mashariki. 

Aidha aliahidi kuiendeleza kazi hiyo ili kuiwezesha nchi kupiga hatua kiuchumi kwa kuimarisha uchumi na fursa kwa vijana na Taifa kwa ujumla. 

Pia alisema kuwa miongoni mwa vipaumbele vyake kama atachanguliwa na Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mwakilishi wao atahakikisha nchi zinafanya biashara bila vikwazo ili kuweza kuwanufaisha wananchi. 

Kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi alichukua fomu ya kugombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA)katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo jijini Dodoma akisindikizwa na makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.  

Chikulupi Njelu Kasaka ambae kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili, ni mbobezi wa masuala ya siasa, utawala na diplomasia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mahusiano ya kimataifa na diplomasia. 

Chikulupi amekitumikia Chama Cha Mapinduzi katika nyanja tofauti na pia ni mjumbe katika kamati mbalimbali. 

Naye Mgombea wa ubunge Wabunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mariam kangoye alijitokeza kuwania nafasi hiyo huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika chama cha Mapinduzi (CCM).  

"Leo hii nimekuja kuchukua fomu baadaya ya taarifa iliyotolewa na katibu wa bunge,nimeona kwamba nafasi hii nifursa kwangu sababu ninaamini kuwa ninauwezo na pia nitahakikisha nikipata nafasi hii nitaitumia kwa maslahi ya watanzania,"alisema.  

Uchaguzi wa Mwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki unakuja baada ya siku chache mwakilishi wa jumuiya hiyo kufariki dunia Juni, 2024.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com