METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, February 5, 2024

RC MNDEME ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 7 YA MIRADI YA MAJI SHINYANGA

Wakandarasi wa Miradi ya Maji Mkoani Shinyanga wametakiwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuzingatia matakwa ya mkataba ikiwemo kununua vifaa imara hasa mabomba yanayotumika kusafirisha maji kwenda kwa wananchi.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mdeme katika Hafla ya Utiaji saini wa mikataba 7 ya miradi ya Maji uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Ambapo amesema,Miradi yote iliyosainiwa ikamilike ndani ya muda wa mkataba na iwe kwa viwango sawa na thamani ya fedha iliyotolewa.

Katika hatua Nyingine Mdeme amewataka Wakuu wa wilaya kutoa Ushirikiano kwa Wakandarasi ili kukamilisha malengo ya mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ya kuwapa huduma bora ya maji Wananchi.

Akitoa taarifa ya mikataba hiyo Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Mkoani Shinyanga RUWASA Mhandisi Juliet Payovela amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imepanga kutumia Billion 28.9 kwaajili ya utekelezaji wa miradi 33 ambapo miradi 14 ya ukamilishaji ,miradi 15 mipya inajengwa na miradi 4 ya kutafuta vyanzo vya maji na usanifu.

Mhandisi Juliet ameongeza kuwa katika kipindi cha Julai hadi December 2023 RUWASA imeshatangaza jumla ya zabuni 9 ikihusisha ujenzi wa miradi 8 na zabuni 1 kwaajili ya bomba na vifaa mbalimbali kwaajili ya ujenzi wa miradi na kwamba zabuni 7 tayari zimekamilika ambazo zimetiwa saini leo yenye thamani ya shilingi Milioni 6.4.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Geospatial Classic Works Ltd Stephen Owawa kwa niaba ya Wakandarasi waliosaini mikataba hiyo amesema , wamepokea maelekezo na kwamba watatekeleza kazi yao kwa ufanisi kama mkataba ulivyoelekeza.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com