METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 6, 2023

Mkandarasi Tanga Akalia Kuti Kavu//Naibu Waziri Kapinga Amtaka Kukamilisha Mradi wa Umeme kwa Wakati

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga akizungumza na Wakazi wa Kata ya Makuyuni Kijiji cha Sharaka Wilaya ya Korogwe Vijijini alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini, tarehe 6 Desemba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga akiwa na  Watoto wa Hamasa waliofika kumlaki katika Kata ya Makuyuni Kijiji cha Sharaka Wilaya ya Korogwe Vijijini alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini, tarehe 6 Desemba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga akiwa na  Watoto wa Hamasa waliofika kumlaki katika Kata ya Makuyuni Kijiji cha Sharaka Wilaya ya Korogwe Vijijini alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini, tarehe 6 Desemba, 2023.
Wakazi wa Kata ya Makuyuni Kijiji cha Sharaka Wilaya ya Korogwe Vijijini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini, tarehe 6 Desemba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga akizungumza na Wakazi wa Kata ya Makuyuni Kijiji cha Sharaka Wilaya ya Korogwe Vijijini alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini, tarehe 6 Desemba, 2023.
Mkandarasi wa Kampuni TONTAN, Mhandisi Lomayan Mollel akiwaeleza Wakazi wa Kata ya Mbuyuni namna atakvyokamilisha Mradi wa Usambazi Umeme katika Kijiji hicho, Wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga tarehe 6 Desemba 2023, Wilayani Korogwe Vijijini Mkoani Tanga.

Na Zuena Msuya-Tanga

Naibu Waziri wa Nishati  Mhe.  Judith Kapinga  amewataka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kutobeba changamoto za wakandarasi wabovu na wanaolegalega katika kutekeleza Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini  badala yake wawachukulie hatua kwa mujibu wa mikataba uliowekwa.

Mhe. Kapinga amesema hayo tarehe 6 Desemba, 2023 wakati wa ziara yake mkoani Tanga ya kukagua Maendeleo ya Miradi ya Usambazaji wa Umeme Vijijini katika Wilaya ya Korogwe, ambapo pamoja na mambo  mengine ameeleza kuwa REA na TANESCO wakibeba changamoto hizo, inasababisha wananchi kufahamu kuwa wao ndiyo wenye matatizo.

Mhe. Kapinga amelazimika kusema hayo kufuatia kuwepo kwa mkandarasi wa Kampuni ya TONTAN kutounganisha umeme katika baadhi ya vijiji na vitongoji vya  Wilaya ya Korogwe Vijijini kwa sababu mbalimbali.

Amesema Serikali imejitahidi sana kumsimamia huyo mkandarasi, imekaa naye mara nyingi ili kuona atamaliza lini kazi, lakini mkandarasi analegalega na siyo muungwana kwa sababu amepewa kazi ya kuunganisha watanzania ambao wanamahitaji ya umeme ili kuboresha hali zao za kiuchumi na bado ameendelea kulegalega  hivyo hawatendei haki watu hao kwa sababu wanataka umeme ili waboreshe maisha yao.

"REA na  TANESCO acheni kubeba changamoto za wa kandarasi wabovu na wanaolegalega kwa kuwa wananchi wanaona kuwa ninyi ndiyo wenye shida, msiwakingie vifua wala kuwatatulia changamoto zao hayo siyo matatizo yenu ni matatizo ya mkandarasi asiye muaminifu na hatutakubali  mkandarasi mbovu aturudishe nyuma" Amesema Mhe Kapinga

Mkandarasi huyo alitakiwa kumaliza kazi desemba  30 mwaka huu, lakini mpaka sasa takribani siku 24 zimesalia mkandarasi huyo bado hajamaliza kazi, hivyo amewataka REA kutompa kazi tena Mkandarasi huyo hata kama atamaliza kazi hiyo kwa muda uliosalia na Serikali iko kazini kuhakikisha mkandarasi huyo anatekeleza kazi yake kwa mujibu wa mkataba.

Amewataka Wakandrasi kuacha tabia ya kusingizia mvua, barabara mbovu ama eneo la milimani kwakuwa wakati wakipewa mkataba wa kazi hayo yote yalifahamika.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com