Na Saida Issa, Dodoma
KAMPUNI ya shule soft imezishauri shule zote nchini ambazo hazijajiunga na mfumo wa shule soft kujiunga ili kuweza kumpunguzia mhasibu mzigo wa kazi kwa kutumia Teknolojia.
Alisema kuwa kupitia mfumo wa shule soft mzazi anaweza kulipa ada kupitia simu na pia mhasibu kupokea malipo moja Kwa moja kwa njia ya control namba na kutoa risiti ya TRA ambapo pia itasaidia kuongeza Pato la Nchi.
Hayo yameelezwa na Afisa wa fedha wa kampuni ya shule soft Upendo Onesmo katika mkutano wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika Jijini Dodoma.
"Kupitia mfumo huu Kwa kiasi kikubwa inasaidia kuongeza Pato la Nchi na kupunguza faini ambazo zinapigwa na Mamlaka husika na kupata taarifa sahihi,
Vilevile kulikuwa na changamoto moja ambayo karibia shule zote walikuwa wanapitia pale ambapo mzazi anamsomesha mtoto na ikatokea mzazi akapata changamoto ya kifo au ulemavu wa Kudumu hii ni ngumu sana Kwa shule kumfukuza mtoto kwaiyo kinachotokea pale shule inakuwa inamsomesha mtoto bure,
Sasa tulichokifanya tumeweza kujiunga na Insurance Company inaweza kumsaidia yule mzazi pale ambapo amefatiki au anapata ulemavu wa Kudumu na mtoto anaendelea kusomeshwa moja Kwa moja na insurance company kupitia shule soft na akasoma mpaka akamaliza,"alisema.
Alisema kuwa kupitia shule soft mzazi anaweza kuona taarifa za matokeo ya mwanafunzi,taarifa za ada pamoja na matangazo yanayotolewa na shule anayosoma mtoto.
"Tumeweza kumsaidia mzazi kuongeza uhusiano wa mzazi na shule,mzazi atapokea matokeo kupitia mfumo huo na anaweza akatoa maoni ambapo akitoa maoni yake yanafika moja Kwa moja mpaka shule,
Maoni hayo yatamfikia mwalimu wa SoMo husika,Mwalimu Mkuu wa shule pamoja na Mwalimu wa darasa na hii itapelekea Mwalimu na mzazi kusaidia kuona ni namna gani wanamsaidia mwanafunzi na afanye vziri katika masomo na kuongeza idadi ya watu ambao watalisaidia Taifa letu mbeleni,"alisema.
Shule soft ni mfumo ambao unapatikana mtandaoni (online) pale ambapo shule inatakiwa kujiunga inatakiwa kuwa na Mtandao(internet)pamoja na kifaa ambacho kinaunganisha na mtandao huo (internent) mfano Komputa mpakato,simu ya mkononi au kishkwambi na aina nyingine ya vifaa vya kielektroniki ambayo vinaweza kutumika.
Mfumo ukiwa uko sawa inaweza ikatumika ni sawa na wazazi wanavyotumia Mitandao ya kijamii kama Facebook,watsap na Mitandao mingine ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment