MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida Ahmed Misanga amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imewekeza katika kujenga madarasa bora, kuajiri walimu na kulipia gharama za masomo ili wanafuzi wapate elimu bora bila ya malipo.
Misanga ameyasema hayo wakati akizungumza katika mahafali ya Shule ya Sekondari Urughu -TAMSIA wilayani Iramba ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita inavyowekeza katika moundombinu ya elimu sambamba na kutoa elimu bure.
"Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imewekeza katika kujenga Madarasa bora, kuajiri walimu na kulipia gharama za masomo ili wanafuzi wapate elimu bora bila ya malipo.
Kuhusu wanafunzi wanaojiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwishoni mwa Novemba Misanga amewatakia ufaulu wanafunzi.
Pia amewashauri walimu na wazazi kusimamia elimu na malezi bora kwa wanafunzi ili wapate ufaulu wa juu katika masomo yao na kuwa vijana wenye maadili, tabia nzuri na wenye hofu ya Mungu katika jamii.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi kuwa na nidhamu katika masomo yao kwa kuwa mwanafunzi mwenye nidhamu katika masomo yake, walimu na wazazi siku zote hupata ufaulu wa juu.
Pamoja na hayo amewahimiza walimu na wazazi kuhakikihasha wanawapa wanafunzi elimu ya utunzaji mazingira na upandaji miti kwa vitendo katika maeneo ya shule na kutunza mazingira katika maeneo ya makazi.
Misanga pia ametoa zawadi kwa wanafunzi waliopata ufaulu daraja la kwanza na pili pamoja na wanafunzi wenye nidhamu shuleni na kugawa vyeti vya uhitimu vilivyoandaliwa na shule.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment