Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Hamis Mwinjuma amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphey Polepole Agosti 2, 2023 baada ya kufika nchini Cuba kwa ajili ya kuhudhuria maonesho ya kimataifa ya Michezo ya Havana, yanayofanyika nchini humo na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.
Akiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Naibu Waziri, Mhe. Mwinjuma amejadiliana na Balozi Humphrey Polepole kusaidia mabondia wa Tanzania kubadilishana ujuzi na Mabondia kutoka Cuba, ikiwemo kuwasaidia kuweka kambi nchini Cuba.
Aidha Naibu Waziri, Mwinjuma amepongeza juhudi za ubalozi huo katika kukibidhaisha Kiswahili ambapo wamewezesha kufikia makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo kikuu Cha Havana na Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ambapo Kiswahili kitaanza kufundishwa chuo Cha Havana kuanzia Septemba mwaka huu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment