Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi mitatu ya maendeleo katika sekta ya Elimu kwa kata mbili za Lighwa na Mungaa na kuahidi kupeleka jumla ya shilingi milioni kumi (10) kuunga mkono juhudi za wananchi.
Katika miradi hiyo ameahidi kupeleka shilingi Milioni tatu (3) katika shule ya msingi shikizi ya Sanya iliyopo katika kijiji cha Lighwa kata ya Lighwa jimbo la Singida Mashariki ambayo mwaka 2020 alichangia Bati 30 na serikali ilipeleka kiasi cha shilingi Milioni 12.5 kwaajili ya kukamilisha maboma yaliyojengwa kwa nguvu ya wananchi.
“Nimekuja kuangalia na kukagua matumizi ya fedha tunazozitoa kwaajili ya shughuli za maendeleo kwakweli niwapongeze tutaendelea kutafuta wafadhili lakini piac muendelee kujitolea ili Watoto wetu wasitembee umbali mrefu” Mhe. Miraji Mtaturu mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki
Katika hatua nyingine Mhe. Mtaturu ameahidi kuchangia shilingi Milioni mbili (2) kwaajili kuunga mkono juhudi za wananchi katika ujenzi wa maabara ya Sayansi katika shule ya Sekondari Lighwa iliyopo kata ya Lighwa ambayo kwasasa wamefyatua tofari elfu tatu (3,000) kwaajili ya kuwanza ujenzi
Maabara hiyo ya shule ya Sekondari Lighwa ilianza hatua za ujenzi mwaka 2009 na ilikomea hatua ya msingi kutokana na kukotokuwepo hamasa kwa wananchi katika kuchangia nguvu ya maendeleo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa kata ya Lighwa diwani wa Lkata hiyo Gabriel Mukhandi amemshukuru bunge wa Jimbo hilo Mhe. Miraji Mtaturu kwa kuwa mkombozi wao kwa kuendelea kuwa sauti ya wananchi wa lighwa na Singida Mashariki kwani kwa sasa maendeleo yanaonekana.
Aidha, Mhe. Mtaturu amefurahishwa na mwamko wa wananchi wa Muve-kitunda kwa kufanikisha kujenga maboma ya vyumba viwili vya madarasa ambapo ameahidi kufikia mwezi desemba 2023 atachangia kiasi cha shilingi Milioni tano (5) kwa ajili ya upaiwaji wa vyumba viwili vya madarasa katik shule shikizi ya Muve- kitunda ambayo kabla ya fedha hiyo aliwahi kuchangia kiasi Milioni 1.3 mwaka 2020 fedha ambayo ilitumika kwaajili ya ujenzi wa shimo la Choo.
Mhe Mtaturu amewahakikishia kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuboresha mazingira ya Elimu nchini kwa kuendelea kugharamia Elimu bila malipo na ujenzi wa Miundombinu ya Madarasa,Maabara,Nyumba za Walimu na Matundu ya vyoo.
0 comments:
Post a Comment