Katibu Mtendaji, Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Griffin Mwakapeje akiongoza kikao cha Menejimenti Kilichofanyika Leo Julai 6, Mwaka huu katika ukumbi wa ofisi za tume Dodoma. |
Wajumbe wa menejimenti ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania wakifuatilia kikao. |
|
Kikoa kikiendelea |
KATIBU Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Griffin Mwakapeje amesema Tume hiyo ipo kwenye mchakato wa kutekeleza Mpango wa kushirikisha vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini katika mashindano ya Uandishi wa Insha za masuala mbalimbali ya Kisheria na yenye changamoto katika jamii ili waweze kushiriki na kuchangia katika utaratibu wa marekebisho ya sheria kwenye maeneo husika.
Maelezo hayo ameyatoa wakati wa Kikao Cha menejimenti ya
Taasisi hiyo kilichofanyika leo Julai 6, mwaka huu Katika ukumbi wa mikutano wa
Ofisi za Tume hiyo ambapo ameeleza kwamba yapo matukio mbalimbali yanayoibuka
Katika jamii yenye mueonekano wa kisheria ambapo zikiandikwa Insha zinaweza
kuisaidia Tume kupata taarifa za kitafiti.
Alisema Kazi hiyo ya Uandishi wa Insha kwa wanafunzi itasaidia kuwajengea wanafunzi hari ya
kufanya utafiti na kuiwezesha Tume kupata
taarifa mbalimbali zitakazofanyiwa kazi Kwa kina na wataalamuwa Taasisi
hiyo, Jambo ambalo litaongeza ufanisi wa Tume na maboresho ya sheria.
Aidha alieleza kwamba washindi wa Insha watapatiwa zawadi
mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, kuchapishwa Kwa maandiko yao kwenye
jarida la Tume, pamoja na vyeti na kwamba zoezi hilo litaongeza hamasa kwa wanafunzi kuwa wazalendo Katika
nchi yao.
"Tutafanya
makubaliano na vyuo mbambali hapa nchini kuhusu Uandishi wa Insha ili kuwa na
uratibu mzuri wa zoezi hili ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi kufanya
utafiti wa masuala mbalimbali ya Kisheria yanayogusa jamii ili mwisho wa siku maandiko hayo yasaidie kufanya maboresho ya Sheria husika”,
Alisema Mwakapeje.
Katika kikao hicho, Bw. Mwakapeje aliwahimiza wataalam na
watumishi kuongeza jitahada Katika utekelezaji wa majukumu na kuwataka wawe
wabunifu ili kuyafikia malengo yao.
0 comments:
Post a Comment