Na Saida Issa,Dodoma
SERIKALI imesema kuwa kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya ujenzi wa reli ya Standard Gauge ya Mtwara-Mbamba bay na matawi yake ya kuelekea Liganga na
Mchuchuma.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa alipouliza Je, Mpango wa ujenzi wa Reli ya Kusini umefikia wapi?
"Aidha ataarifa hiyo ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali, ilionyesha kuwa, Mradi huu unaweza pia kutekelezwa kwa utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP),"alisema Naibu Waziri.
Pia alisema kuwa Hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kumuajiri Mshauri wa Kifedha (Transaction Adviser) ili aweze kufanya mapitio ya Upembuzi uliokamilika mwaka 2016 kwa lengo lakuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa mwekezaji kwa utaratibu wa ubia (PPP).
0 comments:
Post a Comment