METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 17, 2023

SPIKA WA BUNGE LA WATOTO AIOMBA SERIKALI KUTENGENEZA MAJUKWAA YA WATOTO


Na WMJJWM, DAR ES SALAAM

Spika wa Bunge la watoto wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani Isfahan Fakhru Bugenyi amewasihi Wazazi, Walezi, Serikali na watendaji nchini kuwatengenezea Watoto majukwa yatakayowawezesha kushiriki  kikamilifu katika masuala yanayowahusu.  

Bugenyi ameyasema  hayo wakati wa Bunge la watoto wa Mikoa hiyo Juni 17, 2023 Jijini Dar  es salaam, ambalo limelenga kuwakutanisha wadau, viongozi wa Serikali na Wizara za kisekta zinazohusika na masuala mbalimbali ya Watoto Ili kujua mahitaji na changamoto zao 

Spika Bugeny amesema majukwaa hayo ni muhimu kwani yataiwezesha Serikali, wadau wa watoto, wazazi, walezi na watendaji kuzingatia kundi hilo wanapopanga mipango Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali itakayosadifu mahitaji halisi na vipaumbele vya Watoto.

 "Lengo la Bunge hili ni kuwatengenezea Watoto Jukwaa la ushiriki wa Siku ya Mtoto wa Afrika  kikamilifu na pia kupaza sauti zao juu ya masuala yanayowahusu Ili kukuza uelewa wao na Jamii kwa ujumla juu ya Haki za Mtoto, Vilevile Bunge la watoto  linalenga kuwakutanisha viongozi wa Serikali, Wizara yenye dhamana na Watoto Ili wasikie mahitaji na changamoto za Watoto Ili wanapo panga mipango na sera, sheria na Miongozo mbalimbali iendane mahitaji halisi na vipaumbele vya Watoto"

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ally Khamis ambaye ambaye ameshiriki ufunguzi wa Bunge hilo amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Watoto wa Wizara hiyo kushiirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya elimu kuhakikisha kila shule inakuwa na Bunge la watoto.

"Tukiwa kwenye shule tunaweza kutafuta kila shule wagombea na kuweza kufanya Bunge la kitaifa na tukalifanya Bunge la Serikali ya watoto na Bunge ilo litawanufaifa watoto wenyewe kijitambua na kujieleza na kuibua changamoto za ukatili na kama kutakuwa na uelewa huu basi tutatokomeza ukatili" amesema Mwanaidi 

Mhe Mwanaidi akatumia fursa hiyo kugusia juu ya suala la watoto na Sheria ya ndoa za utotoni.

"Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kurekebisha vifungu vya sheria ya ndoa taratibu zinaendelea kufanyika kujua umri gani mtoto anatakiwa kuolewa na Umri gani mtoto atakiwi kuolewa" aliongeza Mhe. Mwanaidi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Wakili Amoni Mpanju amewaasa watoto, kutumia fursa za kielimu wanazopewa kama silaha dhidi ya  vitendo vya ukatili katika jamii zao Huku Mkurugenzi mtendaji wa Shirika  la LHRC Dkt. Anna Henga  Akisema Bunge hili la watoto ni sehemu ya kupaza sauti zao na kujadili mambo yanayo wahusu watoto wenyewe.

MWISHO.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com