METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, June 6, 2023

SERIKALI YATIA SAINI MKATABA TATHIMINI YA MAZINGIRA

Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Dkt. Jim Yonaz (kushoto) wakikabidhiana Mkataba wa kufanya Tathmini ya Athari ya Kimazingira na Kijamii kwa ajili ya Ununuzi wa Meli za Uvuvi , Kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ushauri wa masuala ya Mazingira (TANSEQ)  Bwa. Lusako Raphael (kulia) baada ya utiaji saini hafla iliyofanyika Juni 06, 2023 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Dkt. Jim Yonaz  akitia saini Mkataba wa kufanya Tathmini ya Athari ya Kimazingira na Kijamii kwa ajili ya Ununuzi wa Meli za Uvuvi , Kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) wakati wa hafla hiyo.
Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Dkt. Jim Yonaz akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa kufanya Tathmini ya Athari ya Kimazingira na Kijamii kwa ajili ya Ununuzi wa Meli za Uvuvi , Kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) iliyofanyika Juni 06, 2023 katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Dkt. Jim Yonaz akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa kufanya Tathmini ya Athari ya Kimazingira na Kijamii kwa ajili ya Ununuzi wa Meli za Uvuvi , Kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) iliyofanyika Juni 06, 2023 katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ushauri wa masuala ya Mazingira (TANSEQ)  Bwa. Lusako Raphael akitia saini Mkataba wa kufanya Tathmini ya Athari ya Kimazingira na Kijamii kwa ajili ya Ununuzi wa Meli za Uvuvi , Kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) wakati wa hafla hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na; Mwandishi Wetu - Dodoma

Serikali imetia saini  Mkataba wa kufanya Tathmini ya Athari ya Kimazingira na Kijamii kwa ajili ya Ununuzi wa Meli za  Uvuvi , Kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP).

Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo Juni 6, 2023 Jijini Dodoma, Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonaz amesema mkataba huo ,utawezesha kufanyika kwa tathmini ya athari ya mazingira pamoja na  matengenezo ya meli zitakazotumika katika uvuvi wa Bahari Kuu ili  kupata mazao ya bahari yatakayochangia katika uchumi wa Nchi.

Dkt. Yonaz aliendelea kusema kuwa, sambamba na tathmini hiyo  pia utafanyika  upembuzi  yakinifu katika kuundwa kwa vyombo hivyo  kazi itakayofanyika kwa muda wa  siku 75  ambapo itagharimu shilingi   milioni 349 huku akisisitiza  umakini katika usimamizi wa utekelezaji wa kazi hiyo. 

“Tanzania inazo rasilimali nyingi za majini, sasa ili kuhakikisha tunainua uchumi kupitia  Uchumi wa Bluu Serikali imeona ni muhimu kutengeneza meli kubwa zitakazovua katika kina kirefu ili kupata mazao ya bahari ambapo meli nne zitatengenezwa  kwa ajili ya Zanzibar na Meli tano kwa Tanzania Bara hivyo kukamilika kwake kutasaidia kuinua uchumi wa Taifa." Amesema Dkt. Yonazi.

Pia Katibu Mkuu huyo amewahimiza wadau wa uvuvi ambao ni  Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) na Shirika la Uvuvi la Zanzibar (ZAFICO) kushirikian ana Mkandarasi huyo kuhakikisha  kazi hiyo inafanyika kikamilifu huku akihimiza kila mmoja kuwajibika kwa sehemu yake kwa lengo la kupata matokeo chanya.

Kwa  upande  wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ushauri wa masuala ya Mazingira (TANSEQ)  Bw. Lusako Raphael amebainisha kwamba lengo la kufanya tathimini hiyo ni kuhakikisha mradi hausababishi athari hasi katika mazingira na jamii.

“Mradi huu unalenga kuwezesha ununuzi wa meli pamoja na uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata samaki hivyo tunategemea kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wote  kama ZAFICO, TAFICO na Wizara ya Kilimo. Pia kuna mkakati wa kudhibiti athari za mazingira ambao ndiyo utakuwa muongozo wa utekelezaji wa mradi.' Ameeleza Mkurugenzi huyo.

Ikumbukwe kuwa AFDP ni mradi wa Kuendeleza Kilimo na Uvuvi unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ukifadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com