METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 2, 2023

JE,LINI SERIKALI ITALETA MABADILIKO YA SHERIA KUPUNGUZA MICHAKATO MIREFU YA UTANGAZAJI WA BARABARA ZA TARURA NA FEDHA KUSIMAMIWA NA MAMENEJA WA WILAYA?"MBUNGE MSALALA"


Na Saida Issa, Dodoma

SERIKALI imesema kuwa Sheria ya Ununuzi wa Umma imetungwa ili kuweka uwiano mzuri wa haki na ushindani katika Ununuzi wa Umma na hutumika kwa Taasisi zote za Serikali na si TARURA pekee. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri TAMISEMI Deogratus Ndejembi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Msalala Idd Kassim Iddi alipouliza Je, lini Serikali italeta mabadiliko ya Sheria kupunguza michakato mirefu ya utangazaji wa barabara za TARURA na fedha kusimamiwa na Mameneja wa Wilaya. 

"Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa muundo wa TARURA fedha zote za miradi na utekelezaji wake umekasimiwa kwa Mameneja wa Wilaya,

Malipo yote huandaliwa na Meneja wa Wilaya na kutumwa kwa Meneja wa Mkoa kwa ajili ya uidhinishwaji na ulipwaji kupitia mfumo wa Malipo Serikalini (MUSE),"amesema.

Aidha, Ofisi ya Mkoa kwa kushirikiana na Ofisi ya Meneja wa Wilaya itaendelea kufanya tathimini kuhakikisha miradi inafanyika kwa kuzingatia thamani ya fedha ili iweze kukidhi uhitaji wake.

Pia Mbunge Huyo aliomba Serikali kuongeza bajeti katika maeneo ya msalala ili kuendana na uhalisia wa maeneo hayo.

"Kwa sasa tayari kunataratibu zinazofanyika chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kuangalia ni namna gani mgawanyo wa fedha unafanyika hapa Nchini ikiwemo katika Jimbo la Msalala nimuombe Mheshimiwa mbunge awe na SUBIRA na muda si mrefu team hii itawasilisha taarifa yake kwa Waziri wa TAMIISEMI na tutaangalia upya utaratibu wa kupeleka fedha hizo katika meneo mbalimbali Nchini,"amesema Naibu Ndenjembi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com