Na Saida Issa, Dodoma
SERIKALI imesema kuwa Kila mitaala inapobadilika hutenga fedha kwaajili ya kuwafundisha waalimu kujiandaa kwaajili ya utekelezaji wa mitaala mipya.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Aldof Mkenda alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Songwe Philipo Mulugo alipouliza kuwa je, katika mtaala mpya unaoendelea sasa Serikali ipo tayari kuanza kuunganisha walimu wa Serikali na binafsi ili waweze kupata mafunzo Kwa pamoja katika kupata mafunzo hayo?
"Wakati mwingine fedha ambazo zimekuwa zikitengwa huwa zinakidhi tu Kwa waalimu wa umma na sekta binafsi wanapohudhuria wakati mwingine huwa wanajilipia na wakati mwingine wanalipwa na Serikali,
Tutajitahidi kukusanya walimu wote bila kujali wanatoka sekta binafsi au sekta ya umma lakini Kwa kadri bajeti itakayo ruhusu tunaweza tukawalipia hata wale wa sekta binafsi kama hairuhusu tutawaalika wahudhurie katika semina na watapata mafunzo haya bila kuchajiwa chochote,"amesema Prof.Mkenda.
0 comments:
Post a Comment