Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama
Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akiwa na Mbunge wa Kisarawe
Selemani Jafo katika ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya
Kurui.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama
Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akivishwa skafu wakati
alipofika katika kata ya Kurui kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa
kata hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama
Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akimnadi mgombea wa udiwani wa
kata ya Kurui Mussa Kunikuni
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama
Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akipokea mmoja wa wanachama
kutoka vyama vya upinzani
Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo
akizungumza katika ufungaji wa kampeni za udiwani kata ya Kurui
..................................................................................................
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Shaka Hamdu Shaka amemwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe.
Selemani Jafo kwa uchapakazi wake uliotukuka na hivyo amewataka wananchi wa
kata ya Kurui wilayani Kisarawe wasifanye makosa kabisa wahakikishe wanamchagua
Mussa Kunikuni kuwa diwani wa kata hiyo katika uchaguzi utakaofanyika kesho
Januari 13, mwaka huu.
Akifunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kurui Shaka
amesema wananchi watakapomchagua Mussa Kunikuni hapo kesho itasaidia kuleta
maendeleo makubwa katika kata hiyo kwa kuwa atakuwa anaunganisha juhudi kubwa
inayofanywa na Rais John Pombe Magufuli pamoja na Mbunge Jafo katika suala zima
la utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya kata hiyo na wilaya nzima kwa ujumla.
Naye,Mwenyeki wa mkoa wa Pwani ndugu Ramadhani Maneno amewataka
wananchi wa kata hiyo kutofanya makosa katika uchaguzi wa kesho kwani mkoa
mzima wa Pwani umeelekeza jicho lake katika kata hiyo ile kuleta heshima kwa
mkoa wa Pwani.
0 comments:
Post a Comment