METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 3, 2023

DKT. GWAJIMA: AFUA ZA MALEZI NA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO KUINGIZWA KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI




NA JOYCE KASIKI,DODOMA

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Malundo Maalum Dkt.Dorothy Gwajima amewaagiza Makatibu Tawala Wasaodizi wa Mikoa kuhakikisha   afua za  Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)zinaingizwa kwenye bajeti za halmashauri  Ili kuwezesha uuyekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya Malezi,Makuzi ,na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM.

Waziri Dkt.Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Kitaifa wa  Wadau watekelezaji wa Programu Jumuishi ya Kitaifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM  2021/22-2025/26) inayolenga watoto kuanzia umri wa miaka sifuri hadi minane ili wawe na ukuaji timilifu.

Amesema mwakani anataka kuona bajeti kwenye halmashauri na mikoa katika utekelezaji wa Programu hiyo.

“Tutakuwa tunafuatilia hilo kuona halmashauri zilizoingiza kwenye mijadala yao suala la MMMAM ili tuone namna gani PJT-MMMAM inavyozingatiwa katika utekelezaji wake.”amesema Dkt.GwajimaDKT

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com