NA JOYCE KASIKI,DODOMA
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Malundo Maalum Dkt.Dorothy Gwajima amewaagiza Makatibu Tawala Wasaodizi wa Mikoa kuhakikisha afua za Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)zinaingizwa kwenye bajeti za halmashauri Ili kuwezesha uuyekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya Malezi,Makuzi ,na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM.
Waziri Dkt.Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Kitaifa wa Wadau watekelezaji wa Programu Jumuishi ya Kitaifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM 2021/22-2025/26) inayolenga watoto kuanzia umri wa miaka sifuri hadi minane ili wawe na ukuaji timilifu.
Amesema mwakani anataka kuona bajeti kwenye halmashauri na mikoa katika utekelezaji wa Programu hiyo.
“Tutakuwa tunafuatilia hilo kuona halmashauri zilizoingiza kwenye mijadala yao suala la MMMAM ili tuone namna gani PJT-MMMAM inavyozingatiwa katika utekelezaji wake.”amesema Dkt.GwajimaDKT
0 comments:
Post a Comment