METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 10, 2023

MBUNGE WA KARATU AMEFURAHIA KUPITISHWA KWA BAJETI YA KILIMO KWANI INALENGA KUMPA NEEMA MKULIMA


Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE wa jimbo la Karatu Daniel Awakii amesema kuwa kupitishwa kwa bajeti ya Kilimo ya mwaka wa fedha 2023/24 kutasaidia wakulima kwani ni bajeti ya matumaini.

Mbunge huyo ameyasema hayo katika viwanja vya bunge Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa wakulima wengi wanaenda kunufaika na Kilimo Cha umwagiliaji kwani fedha nyingi zimetengwa kwaajili ya kuboresha skimu na mambonde.

"Wakulima wengi wanakwenda kunufaika na bajeti hii ya Kilimo kwani fedha nyingi zimetengwa na zinaelekezwa  katika kuboresha skimu na mabonde ili mkulima aache kutegemea Kilimo Cha mvua pekee,

Mfano Mimi katika Jimbo langu la Babati la karatu wakulima sana wa Kilimo Cha kitunguu na ndio Jimbo la kwanza kusambaza kitunguu kwa Afrika Mashariki lakini vile vile fedha zimeletwa kwaajili ya kuboresha bonde litakalo saidia Kilimo Cha umwagiliaji,"amesema.

Pia ameishauri Serikali kuhakikisha zao la kitunguu linapatiwa soko ili liweze kuonekana kama ni zao la kibiashara zaidi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com