Na Hamis Hussein - Singida
SHIRIKA la Umeme Tanzania TANESCO kwa Mkoa wa Singida Limetoa Sadaka ya Futari yenye thamani ya Shilingi Laki sita kwa Wajane, Yatima, Wazee na watu wengine wenye mahitaji maalum ikiwa ni sehemu yake ya kurejesha kwa jamii.
Hafla hiyo imefanyika Jana April 6, 2023 katika
Msikiti wa Taqwa Mjini Singida kupitia Kitengo cha kusaidia jamii yenye uhutaji
ya Nusrat Al Ummati iliyochini ya ofisi ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida ikiambatana
na ugawaji wa Tende kutoka kwa Mkurugenzi wa Tabligh na Da’awa.
Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa
Singida Afisa Usafirishaji Juma Ally Omary amesema shirika hilo limeitikia wito
wa ofisi ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida ambayo ulilitaka shirika hilo
kuwasaidia kundi watu wenye mahitaji maalum.
“Leo
tuko kwenye jambo mhimu jambo la kuwasaidia wenye uhitaji Sheikh alitufikishia sisi
barua Tanesco Mkoa wa Singida na kwa vile taasisi yetu inashughulika na
kuhudumia jamii na inabidi irudishe kwa jamii na sisi tukaona ndani ya muda huu
mchache tuungane na wenzetu katika mwezi huu wa Ramadhani”
alisema Omary
Afisa huyo ameongeza kwa kulipongeza baraza la Waislamu
Tanzania Bakwata kwa kuwa kiunganishi na Jamii hivyo Tanesco inaunga jitihada
za Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zuberi ya kuwasaidia
wenye uhataji.
Kwa upande wake Afisa Uhusino na Huduma kwa wateja
Bi Rehema Mwaipopo alisema kuwa Shirika hilo la Umeme linaihudumia Jamii hivyo
limeungana na watu wenye uhitaji katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo
aliongeza kwa kuiomba ofisi ya Sheikh wa Mkoa kuliombea shirika hilo ili
liendelee kuwahudumia wananchi.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida Sheikh Issa
Nassor amelishukuru shirika la umeme Tanzania kwa Mkoa wa Singida kwa kuwaajali wenye uhitaji ambapo ametumia
nafasi hiyo kuyataka mashirika na taasisi zingine kuiga mfano kutoka Tanesco wa
kusaidia jamii badala ya kusubiri wadau kutoka nje ya nchi
Sheikh Nassoro alisema kuwa wajane na Yatima ni watu
wa karibu na jamii kwa historia ya ukoo na dini pamoja na utanzania ambapo
aliwataka wadau wengine kusaidia jamii
“
Nawashukuru sana Tanesco Mkoa wa Singida kwa kuwajali wenye uhitaji na nitowe
wito kwa mashirika mengine kama vile viwanda vya mafuta, na taasisi zingine
kuiga mfano wa TANESCO kwa kuwasaidia wajane, Watoto yatima, wafungwa wa
magereza ni aibu yaani hadi waje watu kutoka Uturuki na Misri kuwasaidia ndugu zetu” . Alisema
Sheikh Issa Nassoro.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kitengo cha Kusaidia jamii yenye Uhitaji kama vile Wajane, Yatima na Wazee ambao hawajiwezi cha Nusrati Al Ummati Ally Amani aliishukuru TANESCO Mkoa wa Singida kwa kutoa Futari hiyo pamoja na Taasisi ya Sheikh Arfu ambayo imetoa Tende.
“Mashallah
wapendwa kaka zetu, Wapendwa shirika letu la Tanesco tunashukuru sana kwa
msaada mlitofanyia na tunawaombe mwenyezi Mungu awafanyie wepesi na
kuwatimilizia mahitaji yenu karibuni tena kwenye ofisi ya sheikh Mkuu wa Mkoa
wa Singida. Vilevile tunamshukuru sheikh Arfu na kampuni yake kwa kutulelea
tende kama boksi 20 tunamshukuru sana na
tunamuomba allah amsamehe makosa
yake kheri ya mwenyezi Mungu ziwe juu
yake” . Alisema Amani
0 comments:
Post a Comment