
Kaimu Meneja wa TMDA kanda ya magharibi Kiboko Magigi aliyevaa suti ya Bluu akishuhudia ushushaji wa mabox ya madawa ya aina mbalimbali kwenye eneo la Magereza mkuu wa Uyui na kushuhudiwa na Askari wa vyeo mbalimbali wa jeshi la Magereza wakiongozwa na Kaimu mkuu wa Gereza hilo Dkt Richard Malifedha .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kaimu meneja wa TMDA kanda ya magharibi Kiboko Magigi alisema kwamba dawa zilizokamatwa silikuwa hazipaswi kuunzwa kwenye maduka dawa muhimu.
Alisema kwamba msako wa kukamata dawa hizo ulifayika katika mkoa wa Tabora ,Katavi na Kigoma nakuongeza kuwa dawa hizo hazina madhara kwa matumizi ya binadamu .
Kiboko alisema kwamba kukamatwa kwa dawa hizo kunatokana na kukiukwa kwa kanuni ya 63 ya makundi ya dawa inayo zuia dawa hizo kuuzwa katika maduka muhimu ya dawa.
Aidha kaimu meneja wa TMDA kanda ya magharibi kwa mamlaka waliyopewa wanatakiwa kusambaza dawa hizo kwa vituo vywa watu wenye uhitaji ikiwemo Magereza ambako wanawafungwa ambao wanaea kutuia dawa hizo.
Alisema kwamba dawa hizo imezikabidhiwa kwa jeshi la Magereza mkoani Tabora kwa ajili ya kuwapatia wafungwa ambapo zitawasaida matibabu wafungwa ambao wako katika gereza kuu la Uyui
Akipokea Dawa hizo Kaimu mkuu wa Gereza kuu la Uyui Dkt.Richard Malifedha aliishukuru Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya Magharibi kwa kutoa dawa hizo kwa zahanati ya Gereza hilo hilo.
Alisema kwamba dawa hizo zitakuwa ni msaada mkubwa kwa wafungwa kutokana na uhaba wa dawa ambao umekuwa ukiwakabili mara kwa mara .
Alisema kwamba Gereza hilo linawihitaji wa dawa mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa waliomo ndani ya gereza kuu la Uyui.
0 comments:
Post a Comment