METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 6, 2023

TAMIU YAKUTANA NA BOT KUJADILI UENDESHWAJI WA TAASISI NDOGO ZA KIFEDHA


Na Saida Issa, Dodoma

ZAIDI ya Taasisi 200 za Umoja wa watoa huduma ndogo za Fedha Tanzania (TAMIU) umekutana na Benki kuu ya Tanzania BOT ili kujadili namna ya uendeshwaji wa Taasisi hizo.

Akizungumza Katika Mkutano jijini Dodoma Mwenyekiti Mstaafu wa TAMIU Nyihita Wilfred amesema lengo kuu la kukutana ni kujadili miongozo ya uendeshwaji wa Taasisi hizo.

"Lengo hasa ni wageni kutoka benki kuu kutufundisha na kutuelimisha juu ya miongozo mbalimbali ikiwa wao kama wasimamizi wakuu wa Taasisi hizi za watoa huduma ndogo ya fedha nchini,

Kwaiyo kubwa tumejifunza na wageni wetu walifika wameweza kutufundisha kuhusiana na miongozo mbalimbali na taratibu za kisheria,pia juu ya kanuni na sheria ya mwaka 2019 sheria namba 10 inayosimamia hizi taasisi,"alisema.

Alisema kuwa ili waweze kufanya kazi vizuri ni lazima kuweza kukutana na kuendelea kupata elimu ya namna ya kuziendesha hizi taasisi ndogo za fedha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAMIU Juma Thomas alisema kuwa watahakikisha huduma hizo zinawafika kwa wananchi ambao niwalaji wenye kipato Cha chini kwa kufuata misingi,kanuni na taratibu ambazo zimewekwa na Serikali.

"Wahakikishe wanatoa huduma kwa wananchi wetu ambao ndio walaji wenye kipato Cha chini kwa kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali,"alisema.

Pia aliwataka wakurugenzi kuhakikisha wanachangia ushulu katika halmashauri zao ili kuziinua halmashauri kwani wanapotoa ushuru Pato linaongezeka katika maeneo yao.

"Tunapochangia ushulu katika maeneo yetu tunasaidia kuongeza pato katika maeneo yetu tujitahidi kuunga mkono Serikali yetu hasa pale katika Ujenzi wa miundombinu kama vile Madarasa nk,"alisema

Naye Marry Ngasa Afisa Mkuu katika Idara ya huduma ndogo za fedha Banki kuu alisema wao kama benki kuu niwasimamizi wa Taasisi za huduma ndogo za fedha nawanatoa leseni pia kuangalia utendaji wao katika kusimamia kanuni na sheria zilizowekwa.

"Siku ya Leo tumetoa ufafanuzi katika baadi ya kanuni na baadhi ya mahitaji ya sheria na kanuni zinazosimamia ikiwa ni pamoja na kanuni ya kusimamia huduma ya walaji,"alisema.

Alisema kuwa TAMIU wameeleza mawazo yao na changamoto zao na wao kama benki kuu wamezisikiliza pia walijadiliana Yale ambayo yanawezekana kuweza kufikia muafaka na Kwa Yale ambayo majibu yake hayakupatikana wameyachukia na kuhakikisha wanayafanyia kazi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com