METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 15, 2023

MHE LONDO ATAKA HALMASHAURI NUFAIKA NA FEDHA ZA CSR KUWASILISHA TAARIFA



Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) imezitaka Halmashauri zote nchini zinazonufaika na fedha za uwajibikaji (CSR) kuwasilisha taarifa ya matumizi ya fedha hizo wakati wa kuwasilisha bajeti zao kwa Mwaka 2023/2024.

Agizo hilo limetolewa Machi 15,2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mhe. Daniel Londo baada ya baini mashaka ya matumizi ya fedha hizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

" Haiwezekani Halmashauri inapata Bil. 7 kwa mwaka jana na bado haionekani imefanya kazi gani, hiyo fedha tungeweza kujenga vituo vingapi vya afya, Sasa sio Halmahauri hii pekee Halmasahuri zote nchini ziwasilishe taarifa za matumizi ya fedha hizo "Amesema Mhe. Londo

Sambamba na hilo ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuimarisha usimamizi na kuongeza kasi katika utekelezaji wa ujenzi wa jengo la utawala ili jengo hilo liweze kukamilika na kuanza kutumika.

Aidha Kamati hiyo imetoa pongezi kwa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini ( TARURA) Mkoa wa Mara kwa kusimamia vizuri ukarabati wa barabara ya Kwangwa- Mkirira na Mwisenge - Nyamlasa.

" Kamati imefurahishwa na ujenzi unaoendelea hapa utekelezaji unaridhisha sana hongereni, na huyu mkandarasi apewe kazi nyingine maana viwango vyake vinaridhisha" Amebainisha Londo

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI) Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa atazungumza na SUMA JKT ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokwamisha ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Tarime.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com