Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwanda akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kwa kutoa maelekezo ya maazimio ya Baraza hilo juu ya kuwapongeza TARURA
Na Fredy Mgunda, Iringa.
WAKALA wa barabara mijini na vijijini (TARURA) Manispaa ya Iringa wamepongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi na uboreshaji wa miundombinu katika sehemu mbalimbali
Wakitoa pongezi hizo madiwani wa kata za manispaa ya Iringa wamesema kuwa TARURA wamekuwa na wakati mzuri kutokana na kufanya kazi kwa bidii katika maeneo mbalimbali.
Awali akizungumza naibu meya manispaa ya Iringa Jully Sawani alisema kuwa TARURA wamekuwa wakifanya kazi nzuri hususani katika kata yake ya kihesa kwa kufanya marekebisho katika kipande Cha barabara kilichukuwa korofi Cha kihesa sokoni
"mi nataka niwapongeze TARURA kwa kweli niwape pongezi wamefanya kazi nzuri Kama tunavyowasikia madiwani hapa kweli mmetenda kazi nzuri mi nilikuwa naangalia utekelezaji wake pale kihesa sokoni kiukweli mmefanya vizuri Sana ushauri tuu mnisaidie kurekebisha kale kakipande kengine kalikobakia maana Kuna makorongo yanayoweza sababisha ajali kutokana na madereva kuyakwepa matuta Yale " alisema
Naye diwani wa kata ya Kitwiru Mh. Muhehe alisema kuwa pamoja na utendaji wa kazi mzuri unaofanywa na wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA Manispaa ya Iringa kwa kuanza uboreshaji daraja la Kitwiru - Isakalilo huku akiiomba TARURA kuweka taa za barabarani ili kudhibiti vitendo vya ukatili na wizi ambao umekuwa ukifanyika katika maeneo yaliyo giza
" Mnafanya kazi nzuri Sana niungane na madiwani wenzangu kuwapongeza lakini pia niwaombe TARURA mtusaidie Kule kata ya ilala hatuna taa za barabarani watoto wanaofanyiwa ubakaji kutokana na giza niwaombe mtusaidie pia katika hili " alisema Muhehe
kwa upande wake Carlos Lunyili kaimu meneja wa TARURA Manispaa ya Iringa alisema kuwa pamoja na mafanikio waliyopata wamekuwa na changamoto ya uifinyu wa bajeti ,upungufu wa watenda kazi pamoja na wananchi kujenga katika miliki za barabara hali inayopelekea kupata changamoto wanapofanya kazi zao
" Mheshimiwa mwenyekiti tumekuwa tukipata changamoto mbalimbali wakati wa kutemda majukumu yetu ufinyu wa bajeti umekuwa ukipelekea kushinda kufanya baadhi ya majukumu kwa wakati ,pia upungufu wa watenda kazi ,pia Kuna wananchi wanaojenga katika Hifadhi za barabara,pia TARURA kutokupewa ofisi " alisema lunyili
Ibrahim Ngwada ni meya wa manispaa ya Iringa alisema kuwa changamoto hizo wamezipokea hivyo wanaahidi kutendea kazi huku akiwataka wananchi kuweka taa nje ya nyumba zao ili kuondoa matendo ya ukatili na wizi licha ya kuwepo kwa changamoto ya kutokuwepo kwa taa za barabarani
" nawapongeza TARURA kwa ufanyaji kazi mzuri Kama walivyosema waheshimiwa Madiwani wenzangu hongereni pia kwa kuanza ujenzi na kuweka kwenye bajeti daraja la Kitwiru - Isakalilo lakini pia nimesikia changamoto ya taa za barabarani kazi hii niwape pia watendaji Kama ilivyo Sheria ya ukitaka kujenga lazima upande miti basi hata kuweka taa uwe hivyo kwa sababu tukiwa wabahili matukio hata hayawezi kuisha niwaombe wananchi waweke taa nje ya nyumba zao mpaka pale serikali itakapofanikiwa kuweka taa katika barabara zetu " alisema Ngwada
MWISHO .
0 comments:
Post a Comment