METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 13, 2023

KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI NA MITAJI YA UMMA YAKUTANA NA MSAJILI WA HAZINA


Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji na mitaji umma leo imekutana na kufanya mazungumzo na ofisi ya msajili wa Hazina jijini dodoma ikiwa na lengo la kujionea kazi mbali mbali zinazofanywa na ofisi yake ikiwepo kutoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha utendaji.

Akiongea leo jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe.Jerry Silaa amesema kamati yake imefanya ziara yake ya kikazi katika ofisi hiyo na imepata ushirikiano mkubwa toka kwa Msajili wa Hazina Bw.Nehemia Mchechu.

“Leo tumekutana na msajili wa hazina( Tresury Register) kujua majukumu, mfumo na muundo wa ofisi yake  tumejifunza mengi na namna bora za kuboresha itendaji..” amesema Mbunge Silaa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com