Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama likiwa kwenye kikao cha Robo ya Pili ya Mwaka kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hapo jana Machi 16, 2023. |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Messos Akizungumza wakati wa Baraza la Madiwani jana. |
Diwani wa Vitimaalum Kata ya Nkinto Florence Yona akiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mkalama. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Asia Messos wakiwa kwenye picha pamoja wakati Kikao kikiendelea. |
Madiwani na waalikwa mbalimbali wakiwa katika kikao hicho. |
Kikao cha baraza la Madiwani kikiendelea. |
Wakuu wa idara na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakiwa kwenye Kikoa cha Baraza la Madiwani kilichoketi jana Machi 16, 2o23. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega akifunga kikao cha Baraza la Madiwani hapo jana. |
Na Hamis Hussein - Mkalama
BARAZA la
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama limemfuta kazi Mtumishi mmoja huku
wengine wawili wakipewa onyo na adhabu mbalimbali kutokana na watumishi hao kukiuka
taratibu na Kanuni za kiutendaji za utumishi wa Umma.
Baraza hilo ambalo
limeketi jana Machi 16, 2023 limepitisha maazimio hayo kwa watumishi hao wa
umma baada ya kupokea malalamiko yanayowakabili watumishi wale ambapo kamati ya
utumishi wa umma imekubaliana kuchukua hatua hizo.
Mtumishi ambaye
amefukuwa ni Elibarick Siasi Ombai ambaye alikuwa mtendaji wa Kijiji cha
Maziliga ambapo kamati imemfuta kazi kutokana na kushindwa kusimamia majukumu
yake na hali ya utoro uliopitiliza.
Mtumishi
Mwingine ni Afisa Elimu Vielelezo wa Halamshauri hiyo Nasibu Mohamed Pangaela ambapo amepewa adhabu ya kushushwa cheo na kubadilishiwa kituo cha kazi wakati akiwa kwenye matatazamio kutokana na utoro kazini.
Na Mtumishi wa
Mwisho ni Nkwangu Musa Nkwangu Aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kidarafa ambaye kwa sasa yupo kijiji
cha Msiu, yeye amepewa miezi mitatu kurudisha shilingi 601,000/= fedha mbichi
ambapo mtendaji huyo hakuzipeleka benki fedha hizo na kuzitumia kwa matumizi yake
mwenyewe.
Baadaya kutoa
taarifa ya hatua za kinidhamu kwa watumishi hao watatu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega
amewataka watendaji wa halmashauri hiyo kutekeleza wajibu wao ambapo
amewasisitiza wakuu wa idara kuwaka ratiba za kufanikisha majukumu yao kwa
ufanisi.
“Watendaji Wangu niwaombe sana mjipange
kila mmoja kwa nafasi yake sio lazima tukupe azimio ndio ufanye kazi,
tunatamani kuona kila mkuu wa idara anapanga ratiba yake ya kazi ili ilete
ufanisi yaani siku moja baraza hili tuligeuzi liwe la kutoa hongera na pongezi kwa kila
Mkuu wa idara kwamba mmefanya Vizuri, kwahiyo natamani kuona hivyo sio lazima
tuwe na Maazimio mengi kama kazi inaenda vizuri” alisema Mkwega.
Kuhusu kupunguza
hoja za ukaguzi Mwenyekiti huyo alisisitiza watendaji hao kupitia kamati ya fedha kushirikiana ili hoja hizo ziwe zimeisha ifikapo robo nyingine Mwaka.
“Kwenye kamati yetu ya Fedha suala la
hoja za ukaguzi tumelitolea muda, yale yanayowezekana kufuta hizo hoja zifutwe
kila mmoja kwa nafasi yake hatupendi kuendelea tena kwenye Quarter inayokuja tukutane
na hoja hizo hizo bado zimesimama zilivyo, kila mmoja apambane aone namna
anavyoweza kufuta hoja yake”
aliongeza Mkwega.
Naye Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo Asia Messos amewaeleza Madiwani na watendaji wengine
kuhamisha wakulima kuchukua mbegu za ruzuku za serikali ili walime katika
kipindi hiki ambacho mvua imerejea ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa
Mkoa aliyeagizwa Wakulima kugawiwa mbegu hizo kwa Mkopo.
Aidha kuhusu
ujenzi wa miundombinu ya vyoo katika shule za Chemchem na Miganga Mkurugenzi
huyo alisema kuwa tayari ameshakaa na wakuu wa shule pamoja na watendaji kuona
namna ya kujenga vyoo hivyo hivyo akatumia baraza hilo kuwaomba Madiwani
kuhamasisha wananchi wao kujitolea nguvu zao kukamilisha miundombinu hiyo ili
kuwaweka wanafunzi katika mazingira ya usalama.
0 comments:
Post a Comment