Na GetrudeVangaye,Rahma Hajia. Dodoma
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni ameeleza sababu
zilizo sababisha ajali iliyotokea
wilayani kongwa mkoani Dodoma ikiwemo
uzembe wa madereva kutofata sheria za usalama barabarani ambapo ilisababisha vifo vingi vya watu na majeruhi .
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ila uchunguzi wa
awali unaonesha kuwa chanzo cha
ajali hiyo ni makosa ya kinidhamu yaani uzembe
unaosababishwa na madereva kwa kuacha kufuata sheria na alama za
barabarani
Amesema kuwa serekali imeamua kuchukua hatua ambazo zitaweza kupunguza ajali za barabarani moja kati ya hatua zilizo chukuliwa ni kuangalia mfumo mzima wa utoaji leseni
nchini ambapo utaangazia katika sekta kuu tatu ambazo ni chuo cha mafunzo ya
udereva, dawati la leseni ambalo linasimamiwa
na jeshi la polisi na mamlaka ya
mapato Tanzania(TRA).
‘’Uhakiki wa madereva
utafanyika kwa kuwasajili madereva wote kwenye mfumo wa LATRA hii
itahusisha wanaoendesha magari ya masafa marefu pamoja na malori yanayosafirisha mizigo’’ .
‘’kuanza kwa uparesheni kali ambazo zitahusisha jeshi la polisi
kufuatilia nyendo za madereva usiku na
mchana katika barabara zote kuu,’’amesema Masauni.
Nae Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP)Camillius Wambura ametoa onyo kali kwa askari wa usalama barabarani kumuadhibu bila huruma kwa yoyote atakayepokea rushwa hali inayosababisha madereva kutofata sheria za usalama barabarani.
0 comments:
Post a Comment