METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, January 7, 2023

BASHUNGWA AKUTANA NA VIONGOZI WA CCM MKOA WA MTWARA ASISITIZA MAELEKEZO YA DKT. SAMIA


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa(Mb) wakati akiendelea na ziara ya kikazi ya Kawaida katika Mkoa wa Mtwara alipata nafasi ya kupita katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoani hapo kwa ajili ya kusalimia na kusaini katika kitabu cha wageni.

Bashungwa alipokelewa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara na akatumia nafasi hiyo kutoa Salamu za Chama na Serikali kwa viongozi hao. Jana tarehe 6 Januari 2023

Akizungumza na Viongozi wa Chama, Bashungwa aliwakumbusha Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kutekeleza Maelekezo ya Mwenyeki wa CCM Taifa, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akifunga Mkutano mkuu wa 10 uliofanyika Disemba 8, 2022 Jijini Dodoma.

Aidha, Bashungwa alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa wazalendo kwa kutoa ushirikiano kwa Vyombo vya Ulinzi vilivyopo karibu na maeneo yao ili kudhibiti uhalifu wa aina yoyote unaoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi yetu ikiwemo ulinzi wa mipaka kwani wananchi  ni sehemu ya ulinzi wa Taifa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com