METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 6, 2022

WAFUGAJI WATAKIWA KUCHANJA MIFUGO YAO ILI KUTOKOMEZA MAGONJWA YA MIFUGO.


Na Rhoda Simba Dodoma

Mkurugenzi wa huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga ametoa wito kwa madaktari wa mifugo nchini kuhakikisha wafugaji wanachanja mifugo yao ili kutokomeza magonjwa yanayoshambulia mifugo ikiwemo ugonjwa wa sotoka na kichaa cha mbwa.

Prof. Nonga ametoa wito huo wakati akikabidhi chanjo kwa wataalamu wa mifugo jijini Dodoma zilizotolewa na chama cha madaktari wa mifugo nchini TVA zitakazotumika kuchanja mifugo zaidi ya elfu sita ambapo amesema suala la chanjo ya mifugo linapaswa kuwa ajenda ili kutokomeza magonjwa ya mifugo kwa asilimia 70 mpaka ifikapo mwaka 2030.

“Wenzetu hawa wa TVA wametoa hizi chanjo 1100 zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki tatu kwa mapenzi mema ili kuwawezesha wenzetu wakazi wa jiji la Dodoma wanakuwa salama kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa”amesema Prof. Nonga.

Amesema Tanzania kama nchi nyingine zipo kwenye ukanda wa kitropikali ambazo zina joto la wastani zinawezesha vimelea kustawi na kuzaliana kuna mvua na jua kiasi unyevunyevu unaowezesha vimelea ambavyo vinaweza kusababisha maradhi kwa mifugo w kama minyoo fangasi na maradhi mengine.

Amesema Wizara ilichagua magonjwa 13 kama magonjwa ya kipaumbele ikiwemo ya kichaa cha mbwa ambapo amesema mpango wa serikiali nikutomeza kabisa ugonjwa wa sotoka ya mbuzi na kondoo pamoja na kichaa cha mbwa ambapo mpaka sasa uchanjaji wa mbwa bado upo chini kwa asilimia 45.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini TVA Profesa Esron Karimuribo amesema wataendelea kushirikiana na serikali kwa kuzalisha chanjo ya mifugo ili kumaliza magonjwa ya mifugo

“Tunaanza chanjo kesho kwa jiji la Dodoma pembezoni kidogo mwa jiji la katika maeneo ya nala mbalawala lakini pia tutakuja kutoa hadi jiji lengo likiwa ni kutokomeza kabisa kichaa cha mbwa” amesema Karimuribo

 

Nae Profesa Sharadhuli Kimera-Mwakilishi wa chama cha madaktari wa mifugo jumuiya ya madola amesema wao kama madtari wameona kuwa ipo haja ya kuchangia kuboresha chanjo ya kichaa cha mbwa lengo ni mpaka ifikapo mwaka 2030 kuwe na maambukizi sifuri ya kichaa cha mbwa.

“Hizi chanjo 1100 za kichaa cha mbwa na magonjwa ya mapele ngozi tumekabidhi kwakuwa sisi tunaelewa ni wapi panahitaji nguvu zaidi na shirika la afya za wanayama wameweka lengo la kuondoka kichaa cha mbwa cha binadamu kwa maambukizi sifuri Ugonjwa huu Unaathiri kabisa ngozi ya wanayama kwadozi hizi itasaidia kutoa motisha kwa wafuagaji kwakujali masilahi ya wafugaji "amesema Profesa Kimera

Hata hivyo chanjo hiyo imezinduliwa katika tarafa za Nala na Mbalawala ambapo dozi 4000 zitatolewa kwa mbuzi na kondoo ili kuwakinga na ugonjwa wa sotoka.

Mwisho
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com