METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, November 11, 2022

MWAKILISHI WA KAIMU MKURUGENZI WA TPHPA DKT. OSHING SHILLA AWAAGA WANAMICHEZO KUELEKEA MASHINDANO YA SHIMMUTA YATAKAYOFANYIKA JIJINI TANGA



Picha za matukio mbalimbali katika Hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka hiyo yaliyopo Ngaramtoni jijini Arusha. 









Na Innocent Natai: WazoHuru Arusha  

Leo Novemba 10, 2022 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania  Dkt. Oshing Shilla amewaaga wanamichezo watakao iwakilisha mamlaka hiyo katika mashindano ya mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania ( SHIMMUTA), jumla ya wanamichezo 51 na viongozi 4 watarajia kusafili tarehe 13 novemba, 2022 kuelekea Jijini Tanga ambapo mashindano hayo yatafanyika, Mashindano ya Shimmuta yataanza tarehe 14 novemba, 2022 na kumalizika tarehe 29 novemba 2022.

Dkt Oshing Shilla amewaomba wanamichezo kudumisha nidhamu na kujituma na kuakikisha wanarudi na makombe kwa kuwa watumishi wote wa mamlaka wanawategemea.

Mwenyekiti wa michezo Dkt Mohamed Mpina amemuakikishia Dkt Oshing Shilla kuwa jinsi wanamichezo walivyofanya mazoezi matarjio yao ni kurudi na makombe kwani mwaka jana walifanikiwa kupata makombe matatu kombe la Karata, kombe la kukimbia kwa gunia pamoja na kombe la mchezo wa kurusha vishale kwa wanawake, pia amemueleza Dkt Oshing Shilla kuwa mwaka huu watashiriki mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa mikono, kukimbia kwa gunia, kuvuta kamba, karata, mchezo wa kurusha vishale pamoja na kukimbia mbio za mita 100, 1500, na  3000. 

Katika hafla hiyo Dkt Oshing Shilla kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi amewakabidhi wanamichezo jezi za mamlaka zitakazo tumika katika mashindano hayo poamoja na Mipira.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com