Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa leo tarehe 11 Novemba 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi.
Katika Mazungumzo hayo, yaliyofanyika Unguja, Mjini Zanzibar, Waziri Bashungwa ametumia nafasi hiyo kumueleza mwenyeji wake kuhusu shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini kuhudumu katika baraza lake la mawaziri.
Pia, Waziri Bashungwa amempongeza Rais Mwinyi kwa kutimiza miaka miwili tangu alipoingia madarakani kuiongoza Zanzibar huku kukiwa na mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu y serikali na matakwa ya wananchi wa Zanzibar ikiwemo kuakisi kwa vitendo tafsiri ya uchumi wa Bluu.
Waziri Bashungwa amesema kuwa Rais huyowa Zanzibar ameonesha mwelekeo mzuri kwa kutekeleza kwa kasi ahadi za maendeleo endelevu kwa wananchi wa Zanzibar na kuwa mtetezi wa wananchi wanyonge ikiwa ni pamoja na ongezeko la Uwekezaji na Watalii.
Kadhalika, Waziri Bashungwa amemshukuru na kumpongeza Rais Mwinyi kwa kuhudumu wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa miaka 11 huku akiahidi kuendelea kusimamia misingi aliyoianzisha kwa manufaa ya ustawi wa nchi na ustawi wa Muungano.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment