Na Mathias Canal,
WEST-Geita
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amepongeza kasi ya ujenzi wa Chuo cha
Ufundi stadi-VETA katika mkoa wa Geita.
Ametoa pongezi hizo leo
tarehe 10 Octoba 2022 wakati akizungumza na uongozi wa VETA mara baada ya
kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa VETA akiwa katika ziara ya kikazi
mkoani Geita.
Pamoja na pongezi hizo
Waziri Mkenda ametaka usimamizi madhubuti wa ujenzi wa vyuo hivyo ikiwa ni
pamoja na kusimamia ubora wa stadi na ufundi zitolewazo katika vyuo hivyo.
Waziri MKenda amesema
kuwa kazi ya usimamizi wa ujenzi kimepewa chuo cha ufundi Arusha hivyo
wanapaswa kusimamia kazi iende vizuri na kukamilisha ujenzi haraka.
“Mkifanya vizuri
tutawasifu, sisi sio kazi yetu kuwaponda ila tunataka kazi iende na kwa hapa
Geita hongereni mnaendelea vizuri na chuo cha ufundi Arusha nataka nione
wanabadilika na kama wasipobadilika tutawabadilisha” Amekaririwa Waziri Mkenda
na kuongeza kuwa
“Nawapongeza kwa kubaini
changamoto za ujenzi na hatimaye kurekebisha kadhia hizo, na nimeagiza
Menejimenti, Wahandisi na wataalamu kutoka chuo cha Ufundi Arusha ambao ndio
wasimamizi wa mradi huu waweze kwenda Simiyu na Geita kukagua ujenzi wa VETA”
Waziri Mkenda amesema
kuwa kazi hizo walizopewa chuo cha ufundi Arusha ni kipimo chao hivyo wanapaswa
kusimamia kwa uadilifu na umakini mkubwa na endapo wasiposimamia ipasavyo
Wizara itachukua hatua abazo ni kubwa.
Kuhusu mpango wa kujenga
kampasi au chuo kikuu cha madini, Waziri Mkenda amesema kuwa Wizara yake
inaunga mkono mawazo hayo na kwa kuwa kanda ya ziwa ni kitovu katika sekta ya
madini hivyo haitakuwa vibaya chuo hicho kujengwa kanda ya ziwa.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment