Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini Elia Kidavile akizungumzia umuhimuwa vijanawa chama chama mapinduzi kujitengemea kiuchumi
kaimu afisa Tarafa ya Pawaga Emmanuel Ngabuji aliwapongeza vijana kumuunganga mkono Rais Samia
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa Vijijini inakusudia kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ngazi za kata ili kujiimarisha kiuchumi na kuwa sehemu ya wachangia wakuu wa maendeleo
Akizungumza na vijana wa kata ya Ilolo Mpya,Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini Elia Kidavile, alisema kuwa jumuiya hiyo inapaswa kuwa na miradi yake kila kata ili kuondoa ombaomba ya kila mara kwa wadau walewale kila siku.
Kidavile alisema kuwa ndoto ya uongozi wake ni kuifanya jumuiya hiyo kuinuka kiuchumi kila kata na kuwa na miradi ambayo inaweza kutelezwa kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.
"Natamani jumuiya hii ya Iringa vijijini tuweze kujitegemea kwenye matukio mbalimbali ya chama na umoja huo ili kuondokana na ombaomba anayo kila mara tunaenda kwa wadau walile"alisema kidavile
Alisema kwa kuanza watapokea maoni ya vijana katika maeneo husika ili waweze kupendekeza aina ya miradin wanayoihitaji kulingana na jiografia ya maeneo hayo.
Lakini pia mwenyekiti huyo wa UVCCM Iringa vijijini aliwapongeza vijana wa kata ya Ilolo Mpya kwa kujitolea kuchangia kokoto mchanga na nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya sekondari William Lukuvi ikiwa ni sehemu kuunga utekelezwaji wa ilani ya CCM katika kuboresha elimu nchini
Kwa upande wake kaimu afisa Tarafa ya Pawaga Emmanuel Ngabuji alisema kuwa Umoja wa Vijana Kata ya Ilolo mpya umewasilisha kwa vitendo shukrani zao kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo hayo
Ngabuji alisema kuwa zaidi ya Milioni mia sita (600,000,000) zimetolewa kwenye tarafa ya Pawaga kwa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali za sekondari ambapo imewapunguzia wananchi kuchangia kwenye ujenzi wa madarasa hayo.
Alisema kuwa vijana wanatakiwa kuipenda nchi yao na viongozi wanaowaongoza kwa kuwa wamekuwa wakionyesha njia ya kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
Ngabuji alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa watanzania na kuomba watanzania waendelee kumuunga mkono.
Aloice Mkongo na anord masagari ni vijana wa jumuiya hiyo ya UVCCM wilaya ya Iringa vijijini wameamua kujitolea kuchangia shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari William Lukuvi kutoka na kazi nzuri ya kimaendeleo ambayo imekuwa unafanywa na Rais Samia.
Akitoa neno la shukrani kwa vijana hao waliojitolea katika kuchangia ujenzi wa madarasa na Ofisi Kaimu mkuu wa shule ya Sekondari Wiliam lukuvi Abisai Ugi amesema hatua hiyo imesaidia pakubwa kufanikisha mradi huo
0 comments:
Post a Comment